Na Daudi Manongi-
MAELEZO.
Halmashauri za Miji na Wilaya nchini zimekumbushwa
kukamilisha zoezi la upatikanaji wa madawati kwa shule za msingi na sekondari
ifikapo Juni 30 mwaka huu,2016 ili kutekeleza agizo lililotolewa na Rais Dkt. John
Pombe Magufuli.
Rai hiyo imetolewa leo,May 26,2016 na
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Rebecca Kwandu wakati wa mahojiano na mwandishi
wa habari hizi kuhusu uchakavu wa madarasa na ukosefu wa madawati unaozikabili
shule za kinesi A na B zilizopo wilaya ya Rorya mkoani Mara.
“Suala la upungufu wa
madawati na uchakavu wa madarasa ni changamoto ya kitaifa na kwamba
lilishatolewa agizo na mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kuhusu halmashauri
zote nchini kuhakikisha ifikapo Juni 30 mwaka huu kila mwanafunzi anaketi
kwenye Dawati” Alisema Kwandu.
Kwa mujibu wa Gwandu
alisema Serikali ya awamu ya tano imepania kuinua kiwango na ubora wa elimu
nchini kupitia mikakati na sera ya elimu bure nchini kote.
Aliongeza kuwa hatua
hiyo imeibua changamoto kubwa kwa wanafunzi wengi kujitokeza kwa asilimia kubwa
na hivyo ni wajibu wa halmshauri hizo kukidhi mahitaji ya madawati ili wasome
katika mazingira mazuri.
“Mpaka sasa Serikali
imeendelea kutoa pesa kwa ajili ya elimu bure nchini kote na kumekuwepo kwa
changamoto mbalimbali kama upungufu wa walimu,madawati na madarasa ambapo
serikali inafanya jitihada za kila namna ili kutatua changamoto hiyo”
Akifafanua zaidi Gwandu
alisema Serikali inaandaa harambee mbalimbali na kuongeza wigo wa utoaji wa
vibali vya kuchangia maendeleo ya elimu kwa hiari ili kutoa nafasi kwa wadau mbalimbali wenye nia ya
kufanya.
|
No comments:
Post a Comment