UTUMBUAJI MAJIPU :-DC Ngara awasimamisha kazi Watumishi watano wa Halmashauri kwa ubadhilifu wa Sh 15 milioni. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, March 20, 2016

UTUMBUAJI MAJIPU :-DC Ngara awasimamisha kazi Watumishi watano wa Halmashauri kwa ubadhilifu wa Sh 15 milioni.

Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera,Bi Honoratha Chitanda akibadilishana Jimbo na Mbunge wa Jimbo la Ngara,Mhe.Alex Gashaza.

Na Shaaban Ndyamukama –NGARA. 


Watumishi watano wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera wamesimamishwa kazi kwa ajili ya uchunguzi wa ubadhilifu wa Sh15 milioni,  zilizotolewa kwa ajili ya Sacos ya vijana na umoja wa bodaboda wilayani Ngara.

Mkuu wa wilaya ya Ngara, Bi.Honoratha Chitanda amesema hayo  jana kwenye kikao cha watumishi wakati wa kutoa tathmini ya ziara ya waziri mkuu wa Tanzania,Mhe Kasimu Majaliwa wiki hii wilayani Ngara,Mkoani Kagera na kutekeleza maagizo yaliyotolewa kiutendaji.

Bi Chitanda amewataja watumishi hao kuwa ni Helen Mkongwa ambaye ni Afisa Maendeleo ya jamii, Moses Chegele ,Mwenyekiti wa Vijana Ngara Saccos, Zera Ruben Mhasibu wa Ngara vijana Saccos  na Mary Parangjo, mtia saini na Cosmas Rubangula wa Idara ya Ardhi anahusika kuuza viwanja nyakati za usiku.  


Amesema wahusika hao wanafanya kazi idara ya maendeleo ya jamii kitengo cha vijana pia fedha hizo zilitolewa Januari Mwaka huu na kuingizwa benki akaunti ya Vijana Saccos, kisha kuondolewa kwa kila mmoja kuchukua kiwango chake.


Licha ya kusimamishwa kazi kwa uchunguzi, wametakiwa kutoa maelezo  jeshi la polisi na kulipa fedha hizo ifikapo Machi 21 saa nne asubuhi,  na kwamba Afisa ushirika wilayani humo Kurwa Ganashi anatakiwa kuwajibishwa kwa uzembe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad