![]() |
MUFTI ZUBEIR NI NANI?
Sheikh Zubeiri ni Mufti wa tatu wa
kuchaguliwa. Anashika nafasi hiyo kumrithi Mufti Shaaban Issa Bin Simba
aliyefariki Juni 22, mwaka huu 2015.
Mufti Simba alishikia nafasi hiyo
kutoka kwa Mufti wa kwanza, Sheikh Hemed Bin Juma bin Hemed aliyefariki mwaka
2002.
Mufti Zuberi amezaliwa mwaka
1953 mkoani Tanga na amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na
Naibu Mufti wa Tanzania na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa kwa miaka 22. Pia amewahi
kuwa Naibu Kadhi Mkuu.
Kijiji alichozaliwa ni cha
Kwamndolwa Old Korogwe (Tanga). Amewahi vilevile kuwa Mwenyekiti wa
Halmashauri Kuu ya Taifa Bakwata baada ya kuteuliwa na Mufti na Sheikh Mkuu wa
Tanzania, Hemed Bin Jumaa Bin Hemed. Alikuwa msaidizi wa Mufti wa kwanza, Bin
Hemed tangu 1984 hadi 2002..
ELIMU
Mufti Zubeir ana Shahada ya Sheria
na Uongozi wa Dini aliyoipata katika vyuo vya ndani na nje ya nchi. Awali,
alisoma hadi darasa la nane mkoani Tanga. Amesoma pia katika vyuo mbalimbali
vya nchi za Misri na Mombasa nchini Kenya.
Mufti Zubeir vilevile ni Mkuu wa
Chuo cha Kiislamu cha Salafia kilichopo Bunju, jijini Dar es Salaam, chenye
wanafunzi 1,500 na kinachofundisha masuala ya dini kunzia ngazi ya cheti hadi
shahada.
Ushiriki wake katika shughuli za
kijamii ni pamoja na kuwa miongoni mwa wajumbe wa kamati ya kitaifa ya viongozi
wa dini na serikali na pia ni Makamu Mwenyekiti wa Skauti.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo
na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia
tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
Post Top Ad
Friday, September 11, 2015

HISTORIA:-Mjue Mufti mpya wa Tanzania.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
Makala Inayofuata
KAMPENI ZA CCM 2015:-Taswira Picha za Dr Magufuli alivyotikisa Mkoani Mara.
Makala Iliyopita
UCHAGUZI MKUU 2015-TANZANIA:-Kura za ushindi Urais hizi hapa.
Muonekano wa Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
AnonymousDec 10, 2019Viongozi Wilayani Kasulu watakiwa Kuimarisha Usalama Katika Korongo la Bolelo.
AnonymousJun 29, 2019Shirika la Ndege la Tanzania Laanza Safari za Afrika Kusini Leo 28/06/2019.
AnonymousJun 28, 2019
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment