Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitangaza
baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia
kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu,
Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa. Kushoto kabisa ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Ombeni Sefue.
|
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika
picha ya kumbukumbu na wanahabari waliofika kumsikiliza wakati akitangaza
baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015. Kulia
kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu Mhe
Majaliwa Kassim Majaliwa. Kushoto kabisa walioketi vitini ni Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sefue..BOFYA
HAPA KUONA PICHA ZAIDI
|
BARAZA LA
MAWAZIRI
Wizara ya
Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.
Mawaziri -
George Simbachakene na Angella Kairuki.
Naibu Waziri
- Sumeilam Jafo. Naibu.
Wizara ya
Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira.
Waziri -
January Makamba
Naibu Waziri
– Luhaga Jerrson Mpina
Ofisi ya
Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu.
Waziri -
Jenista Muhagama
Ma-Naibu Waziri –
Dkt. Possy Abdallah na Anthony Mavunde.
Wizara ya
Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Waziri -
Mwigulu Nchemba
Naibu Waziri
- William Ole Nasha
Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Waziri - Bado
hajapatikana.
Naibu Waziri
– Inj. Edwin Ambandusi Ngonyani
Wizara ya
Fedha na Mipango.
Waziri - Bado
hajapatikana.
Naibu Waziri
- Ashantu Kizachi
Wizara ya
Nishati na Madini.
Waziri -
Prof. Mwigalumi Muhongo.
Naibu Waziri
- Medalled Karemaligo.
Wizara ya
Katiba na Sheria.
Waziri -
Harrison Mwakyembe
Waziri wa
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Waziri - Dk.
Augustino Mahiga
Naibu Waziri
– Dkt. Susan Kolimba.
Wizara ya Ulinzi
na Jeshi la Kujenga Taifa.
Waziri - Dk.
Hussein Mwinyi
Wizara ya
Mambo ya Ndani.
Waziri -
Charles Kitwanga.
Wizara ya
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Waziri -
William Lukuvi
Naibu Waziri
- Angelina Mabula
Wizara ya
Maliasili na Utalii.
Waziri - Bado
hajapatikana.
Naibu
Waziri– Inj. Ramol Makani
Wizara ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Waziri
- Charles Mwijage.
Wizara ya
Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi.
Waziri - Bado
hajapatikana.
Naibu Waziri
– Inj. Stella Manyanya
Wizara ya
Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Waziri -
Ummy Mwalim
Naibu Waziri
– Dkt. Hamis Kigwangala
Wizara ya
Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo.
Waziri -
Nape Nnauye
Naibu Waziri
- Anastasia Wambura.
Wizara ya
Maji na Umwagiliaji.
Waziri –
Prof. Makame Mbarawa
Naibu Waziri– Inj. Isack Kamwela
|
Rais Magufuli amefafanua wakati wa Kutangaza baraza hilo kuwa'' -
Kumekuwa na speculation nyingi na watanzania wamekuwa na hamu kubwa ya kujua
baraza la mawaziri, baada ya kusubira kwa muda mrefu, baada ya kuapa tulitakiwa
angalau tarehe kumi tuwe tumetangaza baraza.
Tuliona
angalau tujiridhishe kwanza, baraza lililopita lilikuwa na mawaziri na manaibu
zaidi ya 59, tukaona tuwe na baraza dogo. Hatuwezi kukaa bila baraza, katika
baraza hili, wizara nyingi tumeziunganisha na kutakuwa na wizara 18 na tutakuwa
na mawaziri 19 tu, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri na hazitakuwa na
manaibu waziri.
Lengo ni
kutimiza ahadi yetu ya kuwa na baraza dogo kupunguza gharama na effective kwa
kufanya kazi. Zilitengwa bilioni 2, mawaziri watakapoteuliwa waende semina
elezi, baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza
sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure. Watafanya semina elekezi
wenyewe ndani kwa ndani.
No comments:
Post a Comment