UCHAGUZI ZANZIBAR:-Taswira Picha Mgombea Urais wa CCM Dr. Shein Apiga Kura. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, March 20, 2016

UCHAGUZI ZANZIBAR:-Taswira Picha Mgombea Urais wa CCM Dr. Shein Apiga Kura.

Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Ali Mohamed Shein akipiga kura katika uchaguzi wa marudio  kituo namba 1 cha kupiga kura namba 1 Skuli ya   msingi Bungi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo,March 20, 2016.Picha na Ikulu.
Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika foleni ya wapiga kura ya Uchaguzi wa marudio katika kituo cha kupiga kura Skuli ya msingi Bungi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo,(wa pili kulia) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt.Idriss Muslim Hija, [Picha na Ikulu.]
Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Ali Mohamed Shein  akipokea karatasi ya kupigia kura kutoka kwa PA (1) Jaffar Suleiman  kituo namba 1cha kupiga kura ya Uchaguzi wa Marudio Skuli ya Bungi wilaya ya Kati Unguja zoezi ambalo limefanyika leo,March 20,2016.
Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Ali Mohamed Shein akifanya mahojiano na waandishi wa habari na kuwaonesha kidole kilichoingizwa wino maalum baada ya kipiga kura ya marudio leo katika kituo namba 1cha Skuli ya Msingi Bungi Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Mama Mwanamwema Shein akiiangalia karatasi ya kupigia kura katika uchaguzi wa Marudio baada ya kukabidhiwa katika chumba namba 3 cha   Skuli ya Msingi  Bungi  Wilaya ya kati  Mkoa wa Kusini Unguja, [Picha na Ikulu.]

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad