



![]() |
Maadhimisho
hayo yalipambwa na burudani mbalimbali zikiwemo ngoma na maigizo na kisha
risala zilizosisitiza umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji.
Kwa mujibu
wa shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR hadi sasa kuna wakimbizi kutoka mataifa
mbalimbali zaidi ya 140,000 wanaoishi katika kambi ya Nyarugusu huku katika
kambi ya Nduta kuna wakimbizi takribani 50,000 kutoka Burundi.
Tangu
kufunguliwa tena kwa makambi hayo mwaka jana, mashirika mbalimbali yamekuwa
yakitoa misaada ya kibinadamu katika makambi likiwemo shirika la Oxfam ambalo
linatoa huduma za maji na ujenzi wa vyoo ikiwa ni pamoja na kuwafundisha
wakimbizi namna mbalimbali za kuishi kwa kuzingatia kanuni bora za afya ili
kujilinda dhidi ya magonjwa.
|









No comments:
Post a Comment