Marekebisho
ya ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom ,VPL 2015/2016 yamezingatia mechi za viporo za timu za Azam
FC na Yanga SC zinazoshiriki mashindano ya kimataifa (Ligi ya Mabingwa Afrika na
Kombe la Shirikisho).
Pia ushiriki
wa Azam FC na Yanga SC katika mechi zijazo za mtoano (play offs) zinazokutanisha timu
zitakazotolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, na zile zilizosonga mbele kwenye
Kombe la Shirikisho.
Iwapo Azam
FC itasonga mbele itacheza mechi hizo za mtoano, wakati Yanga SC yenyewe itacheza tu
mechi hizo za mtoano iwapo itatolewa katika raundi inayofuata ya Ligi ya
Mabingwa. Hivi sasa Azam na Yanga zinashiriki hatua ya 16 bora ambayo itachezwa
kati ya Aprili 8-10,2016 kwa mechi za nyumbani, na Aprili 19 na 20,2016 kwa mechi za
ugenini.
Mechi za
kwanza za raundi ya mtoano (play offs) zitachezwa kati ya Mei 6-8,2016 wakati za
marudiano zitafanyika Mei 17-18,2016. Yanga SC ikiitoa Al Ahly maana yake haitacheza
hatua ya mtoano (play offs), na badala yake itasubiri moja kwa moja hatua ya
makundi ambayo mechi zake za kwanza zitafanyika kati ya Juni 17-19,2016.
Marekebisho
mengine yanaweza kufanyika kwa kuzingatia matokeo ya scenario hizo hapo juu.
Wasalaam,
Boniface
Wambura
Ofisa
Mtendaji Mkuu
Bodi ya Ligi
Kuu Tanzania (TPLB)
|
No comments:
Post a Comment