TASWIRA PICHA:Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein Kuapishwa Leo Alhamisi March 24,2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, March 24, 2016

TASWIRA PICHA:Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein Kuapishwa Leo Alhamisi March 24,2016.

Pichani ni Taswira picha ya Maandalizi ya sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa Zanzibar ,Dkt Ali Mohammed Shein, Leo March 24, 2016.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema kuwa sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa Zanzibar , Dk.  ALI MOHAMMED SHEIN zitafanyika leo siku ya Alhamisi Machi 24 katika uwanja wa Amaan, na maandalizi yote yamakamilika  katika shughuli hiyo inayotarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali  akiwemo Rais John Pombe Magufuli pamoja na Viongozi wengine wa kitaifa, katika siku hiyo ambayo pia imetangazwa kuwa ni ya mapumziko kwa upande wa Zanzibar ili kuwapa fursa wananchi kuhudhuria kwa wingi katika hafla hiyo.
Chama cha Mapinduzi Zanzibar ,kimetoa pongezi kwa Rais mteule wa ZANZIBAR Dk.  ALI MOHAMMED SHEIN kwa kushinda kwa kishindo Urais wa Zanzibar  kwa kupata kura Laki  299,982 sawa na asilimia 91.4 katika uchaguzi mkuu wa marudio.


 Uchaguzi huo ambao ulifanyika tarehe 20,March, 2016  ambapo wananchi wa Zanzibar  walipiga kura kuchagua viongozi katika ngazi ya Urais , Uwakilishi na Udiwani

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad