MATOKEO / RATIBA VPL 2015/2016:-Simba SC Yapaa kileleni mwa Ligi Kuu kwa pointi 7 ikishinda wa 2-0 dhidi ya Coastal Union. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, March 19, 2016

MATOKEO / RATIBA VPL 2015/2016:-Simba SC Yapaa kileleni mwa Ligi Kuu kwa pointi 7 ikishinda wa 2-0 dhidi ya Coastal Union.

Wekundu wa Msimbazi ,Simba SC imepaa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa pointi saba zaidi ya wapinzani Azam FC na Yanga SC katika mbio za ubingwa, kufuatia ushindi wa 2 - 0 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga jioni ya leo,March 19, 2016.

 Mchezaji,Danny Lyanga aliifungia Simba SC goli la kwanza dakika ya 39 kipindi cha kwanza kisha Hamis Kiiza akamaliza kazi dakika ya 51 na kupeleka shangwe kwenye mtaa wa Msimbazi.

Simba SC sasa inafikisha pointi 57, baada ya kucheza mechi 24, wakifuatiwa na mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 50 sawa na Azam FC baada ya timu zote hizo kucheza mechi 21. 

Coastal Union iliyozifunga Yanga SC 2 - 0 na Azam FC 1- 0 Uwanja wa Mkwakwani, kipigo cha leo kinawafanya wabaki na pointi zao 19 baada ya kucheza mechi 24 na kuendelea kuburuza mkia katika Ligi Kuu ya timu 16.

Huko Songea, Majimaji FC imeinyuka Mbeya City 2-1 na kushika Nafasi ya 8 wakiwa na Pointi 27 huku Mbeya City wakiwa Nafasi ya 11 na wana Pointi 24 Wakati mchezo wa Stand United na  Ndanda FC wakitoka sare ya bao 1-1.

LIGI KUU VODACOM 2015/2016 – RATIBA. 
                        
Jumapili Machi 20,2016.

African Sports v Tanzania Prisons

Jumatatu Machi 21,2016.

Mgambo JKT v Toto Africans

Alhamisi Machi 24,2016.

African Sports v Toto Africans

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad