CAF CHAMPIONS LEAGUE.:-Yanga SC waitoa APR FC na kusionga Raundi ijayo . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, March 19, 2016

CAF CHAMPIONS LEAGUE.:-Yanga SC waitoa APR FC na kusionga Raundi ijayo .

Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga SC wakiwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Leo March 19, 2016, wakicheza Mechi ya Marudiano ya Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya CAF CHAMPIONS LEAGUE dhidi ya APR FC wametoka Sare ya bao 1-1 na kusionga Raundi ijayo .

Katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa huko Kigali, Rwanda, Yanga SC iliitandika APR Bao 2-1 kwa Bao za Juma Abdul na Thaban Kamusoko.

Donald Ngoma akishangilia na Deus Kaseke baada ya kuifungia bao la kusawazisha Yanga leo,March 19,2016.
Kwenye mchezo wa Leo, Yanga SC walianza vibaya kwa kupigwa Bao Dakika ya 4 tu lakini Donald Ngoma akasawazisha Dakika ya 28 na kuwaingiza Raundi ya mwisho ya mtoano ambayo watapambana na Mshindi kati ya Al Ahly ya Misiri au Recreativo de Libolo ya Angola ambazo nazo Leo zinacheza Mechi ya Pili huko Borg El Arab Stadium Mjini Alexandria Nchini Misri baada kutoka 0-0 huko Angola.
CAF CHAMPIONS LEAGUE.

Raundi ya Mtoano ya Timu 32 – Mechi za Pili

RATIBA/MATOKEO.

**Saa za Bongo.

**Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili

Cnaps Sports – Madagascar 2 Wydad Athletic Club – Morocco 1 [3-6]

Vitalo FC – Burundi 2 Enyimba International FC – Nigeria 1 [3-6] 
   
Young Africans – Tanzania 1 Armee Patriotique Rwandaise FC – Rwanda 1 [3-1]
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza

17:30 AC Leopards de Dolisie – Congo v Mamelodi Sundowns - South Africa

18:30 ES Sahel – Tunisia v Olympique Club De Khouribga – Morocco [1-1] 

19:00 Al Ahly – Egypt v Recreativo de Libolo - Angola [0-0]

21:00 El Merreikh - Sudan v Warri Wolves – Nigeria [1-0]  
  
18:00 Al Zamalek – Egypt v Union Sportive de Douala - Cameroon

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad