CAF KOMBE LA SHIRIKISHO:- Azam FC yasonga Mbele kwa kuichapa Bidvest Wits 4-3. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, March 21, 2016

CAF KOMBE LA SHIRIKISHO:- Azam FC yasonga Mbele kwa kuichapa Bidvest Wits 4-3.

Timu ya Azam FC imefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya CAF Kombe la Shirikisho baada ya kuifunga Bidvest Wits ya Afrika Kusini kwa mabao 4-3 kwenye mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar.

Mabao ya Azam FC yamepachikwa kimiani na Kipre Tchetche aliyefunga mabao matatu ‘hat trick’ na moja likapachiwa na nahodha wa timu hiyo, John Bocco.

Katika mechi ya kwanza, Bidvest ilipoteza kwa mabao 3-0 ikiwa nyumbani Johannesburg. Safari hii imepata mabao matatu lakini ikashindiliwa mengine manne. Maana yake Azam FC imevuka kwa jumla ya mabao 7-3.

 CAF KOMBE LA SHIRIKISHO

Raundi ya Pili.


**Mechi kuchezwa Aprili 08 -10,2016 na Marudiano ni Aprili 19-20,2016.

Vita Club Mokanda [Republic of the Congo] v Sagrada Esperança [Angola]

MC Oran [Algeria] v Mshindi Kawkash Marrakesh/Barrack Young Controller

Azam [Tanzania] v Espérance de Tunis [Tunisia]

Zanaco [Zambia] v Stade Gabèsien [Tunisia]   

CS Constantine [Algeria] v Misr El-Makasa [Egypt]    

FC Saint-Éloi Lupopo au Al-Ahly Shendi v Al-Tripoli au Medeama              

FUS Rabat [Morocco] v SC Villa [Uganda]       

Atlético Olympic au CF Mounana v Africa Sports au ENPPI  
 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad