![]() |
|
TIBA YA
U.T.I NA USHAURI.
Baada ya
kuuchambua ugonjwa wa U.T. I (Urinary Tract Infection ) leo tunazungumzia tiba
yake.
Maambukizi katika njia ya mkojo hutibika kwa dawa mbalimbali za kisasa
baada ya kufanyiwa vipimo na kuthibitika kuwa mgonjwa ana maambukizi hayo.
Dawa ambazo
anaweza kupewa mgonjwa ni kama vile Ciprofloxacin, Monurol, Furadantin, Sulfam
Ethoxazole, Co-trimax, Ampicillin, Gentamicin na kadhalika.
Mgonjwa
anayesumbuliwa na U.T.I hapaswi kutumia dawa yoyote bila kwanza kupata ushauri
wa daktari.
Wanawake
wanashauriwa kuepuka kujisafisha sehemu za siri na maji machafu na yasiyo
salama, pia kuepuka kupaka marashi sehemu hizo, ama kutumia pamba zenye
kemikali ya kukata harufu kwani hizo huua bakteria wa asili wa sehemu za siri
hali ambayo hukaribisha bakteria wa maradhi kuzaliana kwa wingi.
Pia
wanashauriwa wanapojisafisha baada ya kujisaidia kuanzia mbele kwenda nyuma ili
kuepusha kuhamisha bakteria walio eneo la haja kubwa na kuingia njia ya mkojo.
Kwa wale
walio katika kipindi cha ukomo wa hedhi, wanaweza kushauriana na daktari juu ya
kutumia Oestrogen ya ukeni ili kuwasaidia kujikinga na maambukizi ya U.T.I.
Kwa mwanaume
maambukizi haya huathiri nguvu za kiume na kujipenyeza hadi katika korodani na
huathiri uzalishaji wa mbegu za kiume na kunaweza hata kusababisha ugumba.
Hivyo wanashauriwa kuhakikisha wanatibu bila kuchelewa ugonjwa huo.
Pia
maambukizi ya njia ya mkojo huweza kusababisha matatizo ya tezi ya kiume
(prostate) kwani husababisha mrija wa mkojo kuziba, kutopitisha mkojo vizuri na
kuruhusu bakteria kujenga makazi.
Hali hiyo
ikitokea mgonjwa lazima akamuone daktari ili awekewe mrija wa kutolea mkojo.
Tunaweza
kuudhibiti au kuponya ugonjwa huu kwa kunywa maji mengi pamoja na juisi
itokanayo na matunda halisi, iwapo tutawahi kabla tatizo halijawa sugu. Kwa
maana nyingine, unaweza kujikinga na ugonjwa huu kwa kuwa na mazoea ya kunywa
maji ya kutosha kila siku.
Ukinywa maji
ya kutosha yatakufanya uende haja ndogo kila mara na kwa njia hiyo wale
bakteria watakuwa wakitoka na hatimaye kuisha kabisa.
Hivyo basi
ukijisikia unaumwa tumbo chini ya kitovu, joto au maumivu wakati wa kukojoa
mkojo kuwa na rangi ya njano kupindukia na kuwa na harufu kali, kutokwa na
usaha wakati wa kukojoa, kabla au baada ya kukojoa, kutokwa na majimaji katika
njia ya mkojo wakati wa kujisaidia haja kubwa,vichomi katika njia ya mkojo, au
kuhisi kuwashwa sehemu hiyo, kuumwa kiuno, homa kali na kadhalika, nenda
kamuone daktari.Na GPL.
|
Monday, March 21, 2016
AFYA YETU:- U.T.I Ni Gonjwa Linalosumbua Wanawake .
Tags
# DONDOO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
DONDOO
Labels:
DONDOO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.






No comments:
Post a Comment