![]() |
|
Mara baada ya
ajali hiyo na majeruhi kufikishwa hospitali ya wilaya ya Bagamoyo kwa ajili ya
matibabu,Naibu Waziri Jafo alipiga simu kwa menejimenti ya Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili na kuagiza wajiandae kupokea majeruhi wa ajali hiyo kwa Hospitali
hiyo ya wilaya ya Bagamoyo haina uwezo wa kuwatibu.
Majeruhi
waliolazwa katika hospitali ya Taifa ua Muhimbili ni Ibrahim Matovu, Mkurugenzi
Mtendaji wa Wilaya ya Bagamoyo, Juliana Msaghaa, Mhandisi wa Maji wilaya,
Dorothy Njetile, Mratibu wa Tasaf, George Mashauri, Mweka Hazina wa Wilaya,
Amadeus Mbuta, Mshauri wa Tasaf, Julius Mwanganda, Mkuu wa Idara ya Maendeleo
ya Jamii, Tauliza Halidi, Mwananchi na Amari Mohamed, Mwananchi.
Aliyepelekwa
katika hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo na kuruhusiwa ni Grace Mbilinyi ambaye
ni Afisa Utumishi na Utawala wa Wilaya.
Ajali hiyo
ilihusisha lori la mchanga, gari dogo yaliyokuwa yanatokea Bagamoyo kuja Dar es
Salaam, na magari mawili yaliyokuwa kwenye msafara wa Kamati hiyo.
Magari
yaliyokuwa katika msafara wa kamati hiyo, ni gari la Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii (TASAF) na gari la Mkurugenzi wa Wilaya ya Bagamoyo ambayo yaligongwa na
lori hilo la mchanga na kusababisha vifo vya watu hao na kuwajeruhi wengine
kadhaa.Na ITV -TANZANIA.
|
Monday, March 21, 2016
Home
HABARI
MATUKIO
AJALI / PICHA:-Watu watano wapoteza maisha na tisa kujeruhiwa katika ajali ya msafara wa kamati ya Bunge.
AJALI / PICHA:-Watu watano wapoteza maisha na tisa kujeruhiwa katika ajali ya msafara wa kamati ya Bunge.
Tags
# HABARI
# MATUKIO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
MATUKIO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.











No comments:
Post a Comment