MATOKEO / RATIBA EPL 2015/2016:-Matokeo ya Leo March 19, 2016 huku Arsenal sasa Pointi nane nyuma ya Leicester City. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, March 19, 2016

MATOKEO / RATIBA EPL 2015/2016:-Matokeo ya Leo March 19, 2016 huku Arsenal sasa Pointi nane nyuma ya Leicester City.

Mshambuliaji wa Arsenal, Danny Welbeck akifunga bao muhimu kwa  timu yake bao la kwanza katika ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Everton Uwanja wa Goodison Park katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza 2015/2016 jioni ya leo,March 19, 2016. 

Bao lingine la Arsenal limefungwa na Alex Iwobi .

Ni ushindi wa kwanza wa Arsenal katika mechi nne za ligi ya Uingereza na pia Matokeo hayo yanaiweka Arsenal pointi nane nyuma ya viongozi wa ligi Leicester City.

Mabingwa Watetezi Chelsea, wakiwa kwao Stamford Bridge, walisawazisha kwa Bao la Dakika ya 88 la Penati ya Cesc Fabregas na kutoka bao 2 -2  dhidi ya West Ham , waliofunga Bao zao kupitia Lanzini na Andy Carroll .
Habari ya ‘Mujini’ ni Vinara Leicester City kuendelea kuzoa Pointi na kuchanja mbuga kileleni,pale walipoifunga Crystal Palace 1-0 kwa Bao la Riyad Mahrez la Dakika ya 34 ambalo limefungua pengo la Pointi 8 na Timu ya Pili Tottenham.
Kesho Jumapili,March 20, 2016, huko Manchester ndani ya Etihad kati ya Man City na Man united.

Jumapili Machi 20,2016.

1630 Newcastle v Sunderland   
 
1630 Southampton v Liverpool  

1900 Man City v Man United   

1900 Tottenham v Bournemouth


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad