 |
|
Mgombea wa
urais kupitia chama cha CCM Visiwani Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ameshinda
kiti cha urais kwa jumla ya kura 299,982 awa na asilimia 91.4 ya kura zote
halali 328,327 katika uchaguzi wa marudio uliofanyika jana,March 20,2016.
Matokeo hayo
yametangazwa leo,March 21, 2016 na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar
(ZEC) Jecha Salim Jecha.
Uchaguzi huo
wa marudio ulifanywa jana baada ya kufutwa Oktoba 25,2015 kutokana na kile
kilichotangazwa na Jecha kuwa ni kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa taratibu za
uchaguzi huo.
|
 |
|
Uchaguzi huo
ulisusiwa na vyama kumi kwa kile walichodai kuwa kufutwa kwa uchaguzi huo mwezi
Oktoba ilikuwa ni batili.
Hata hivyo
karatasi za kupigia kura zilikuwa na majina yote ya wagombea kama ilivyokuwa
katika uchaguzi mkuu wa Oktoba,2015.
Jecha
alifafanua kuwa hakuna hata mgombea mmoja aliyefuata utaratibu wa kujitoa kwa
mujibu wa sheria na kanuni.
|
Matokeo yote
kama yalivyotangazwa yako hapo
chini....
No comments:
Post a Comment