|
Matukio ya
wajawazito kupoteza watoto kwa madai ya uzembe wa wahudumu wa afya yameendelea
kuugubika Mkoa wa Mwanza baada ya mkazi wa Nyarawambo wilayani Sengerema, Tatu
Muhangwa, kujifungua na mtoto wake kufariki kwa kukosa huduma.
Mama mzazi
wa Tatu, Vumilia Nailon alisema mjukuu wake alifariki baada ya wahudumu wa afya
katika Zahanati ya Ngoma ‘B’ iliyopo Kata ya Nyamatongo wilayani Sengerema,
kuchelewa kumhudumia.
Mhudumu wa
afya aliyekuwa zamu, Helena Mulwisha alisema alishindwa kumhudumia mjamzito
huyo kutokana na kubaini kuwa mtoto alikuwa kakaa vibaya tumboni na kuwashauri
kumpeleka hospitali ya wilaya kwa msaada zaidi.
Nailon
alisema: “Nilimfikisha mgonjwa wangu zahanati juzi, saa kumi na moja alfajiri,
lakini hadi saa tatu hakuwa amepatiwa huduma yoyote hadi alipojifungua mwenyewe
bila msaada na mtoto kufariki.
“Mmoja wa
wahudumu wa afya aliyekuwapo alishindwa kumhudumia baada ya kugundua mtoto
amekaa vibaya tumboni na yeye hana utaalamu wa kumsaidia.”
Alisema
Mulwisha aliwashauri kumpeleka mgonjwa hospitali ya wilaya kwa sababu wauguzi
na madaktari walikuwa wakihudhuria semina.
“Baada ya
kukosa gari ya kumuwaisha hospitali, tuliamua kutembea kwa miguu umbali wa
kilomita mbili, lakini hatukufika baada ya magonjwa wangu kujifungulia njia kwa
msaada wa wasamaria wema na mtoto kufariki,” alisema Vumilia.
Kaimu Mganga
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Dk Henry Nyamete alisema ofisi yake inachunguza
tukio hilo na kwamba itachukua hatua za kinidhamu dhidi ya mhudumu wa afya
aliyekuwa zamu siku hiyo kwa kushindwa kuwajibika kwa kuita gari la wagonjwa
ili kumuwahisha mjamzito huyo hospitali kwa matibabu zaidi.Na MPEKUZI HURU.
|
Monday, March 21, 2016
AFYA YETU:-Kichanga Mwingine Adaiwa Kufariki Dunia Kwa Uzembe Mkoani Mwanza.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.





No comments:
Post a Comment