Mgeni Rasmi
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo akizungumza katika Maombi ya kumuombea
Rais Magufuli, wasaidizi wake pamoja na Taifa yaliyofanyika jana Jijini Mwanza.
Mgeni
Rasmi katika maombi hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ambae
katika hotuba yake, aliwasihi Watanzania wote kuendelea kuliombea Taifa ili
kuondokana na vikwazo mbalimbali ambapo alidokeza kuwa kupitia maombi kama
yaliyofanyika jana, migogoro mbalimbali ikiwemo ya kisiasa kama iliyopo
Zanzibar itamalizika.
Viongozi
mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza Askofu
Charles Sekelwa, Makamu wake Zenobius Issaya pamoja na Kiongozi wa Kundi la
Maaskofu kutoka Jijini Dar es salaam la Good News For all Ministry Askofu
Dr.Charles Gadi pamoja na viongozi wengine wa dini kutoka mikoa mbalimbali
nchini waliliombea Taifa na kuhimiza utuliza nchini.
Wasaidizi wa
wa Rais Maguguli ambao ni pamoja na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu, Waziri
Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu Mhe.Othman Chande, Spika wa Bunge Mhe.Job
Ndugai, Mawaziri pamoja na viongozi wengine wa Serikali wa awamu ya tano
waliombewa ili kuliongoza vema taifa kwa kuendana na kasi ya Rais Magufuli.
Pamoja na
mambo mengine, maombi hayo yalijumuisha toba kwa taifa, kumuomba Mungu
kukomesha mauaji ya Vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na kuombea
taifa mvua zisizo na madhara. |
No comments:
Post a Comment