TAARIFA KWA UMMA:-Studio ya Music ya 'The Industry' Chini ya Producer Nahreel Yamtangaza Rasmi Msanii Mpya wa Kike Aliyejiunga Nao - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, January 14, 2016

TAARIFA KWA UMMA:-Studio ya Music ya 'The Industry' Chini ya Producer Nahreel Yamtangaza Rasmi Msanii Mpya wa Kike Aliyejiunga Nao

THE INDUSTRY MUSIC LABEL
 
TAARIFA KWA UMMA

 UTAMBULISHO WA MWANAMUZIKI MPYA WA STUDIO YA MUZIKI YA “THE INDUSTRY”
 
Uongozi wa Studio ya Muziki ya The Industry iliyoko chini ya Wanamuziki Producer Nahreel na Aika Marealle unapenda kuchukua Nafasi hii kuwatangazia Umma Kuwa kuanzia Tarehe 14 January 2016 Wamemuingiza Msanii mpya wa Kike aitwaye Rosa Ree, Rose Ree ni muimbaji wa Muziki aina ya Rap ambae kazi zake zitaanza kusikika/Kuonekana siku si nyingi kuanzia sasa katika Redio Mbali mbali na TV Stations za Tanzania na nje ya nchi.

 Kama wasikilizaji na watazamani tunaomba Kumuunga mkono Msanii huyu mpya Kwani tuna uhakika hatawaangusha katika kuwaletea burudani Katika Masikio na macho yenu pindi kazi zake zitakapoanza kutolewa hivi karibuni.

The Industry ni studio na kampuni ya muziki ambayo ipo chini ya kundi la music lenye Mafanikio makubwa la Navy Kenzo ikisimamiwa na Producer Nahreel na msaidizi wake Aika Marealle
 
Wasanii Baadhi Waliokwisha fanya kazi na Studio ya The Industry mpaka sasa toka kuanzishwa kwake hivi karibuni ni Diamond Platnumz na wimbo wake wa Nana, Nikki wa Pili na wimbo wa Baba Swalehe, Joh Makini na nyimbo zake kama Don’t Bother na nusu nusu.


Imetolewa na,

The Industry PR

John Kiandika


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad