Afisa
Mawasiliano Mwandamizi wa Bandari ya Tanga(TPA),Moni Jarufu Msemo akitoa neon
la shukrani mara baada ya mkuu wa mkoa wa Tanga,Mwantumu Mahiza kumaliza
kuzungumza na wafanyakazi.
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
IMEELEZWA
kuwa agizo la Rais John Magufuli kusitisha safari za nje kwa watendaji wa
serikali nchini zimesababisha Bandari ya Tanga kufanyakazi chini ya kiwango na
kulazimika kukodi vifaa kwa gharama kubwa nje ya nchi.
Hayo
yamebainishwa na Kaimu Meneja wa bandari ya Tanga,Henry Arika wakati mkuu wa
Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza alipofanya ziara ya siku mmoja kukagua shughuli
zinazofanywa na bandari hiyo.
Alisema kuwa
hatua hiyo ya kusitishwa kwa safari mpaka vibali imechangia bandari hiyo kupata
hasara na kulazimika kukodi Tagi ya kupakuwa mizigo kutoka nangani kwenye meli
hadi katika pwani ya bandari hiyo.
“Mheshimiwa
mkuu wa mkoa japo agizo hilo linafaida kwa serikali lakini tunamuomba
Mheshimiwa Rais angalie upya agizo hilo kwani kuna baadhi ya taasisi
zinazojiendesha kibiashara zinaathirika na utendaji wake wa kila siku
kushuka”alibainisha Kaimu Meneja huyo.
Aliiomba
serikali kuangalia namna bora ya kutenganisha taasisi hizo katika utoaji wa
vibali kwani kwa hili limesababisha kushindwa kupelekaTug meli ya kukokotea
vyombo vya majini yao kwa ajili ya ukarabati nchini Kenya.
“Tagi
tuliyonayo katika bandari ya Tanga ni mmoja pekee na manahoza waliisimamisha
kufanyakazi toka mwezi Novemba mwaka jana hivyo tumelazimika kukodi Tug kutoka
mjini Mombasa ili kurahisisha utoaji wa mizigo”alisema Arika.
Ambapo
aliongeza kuwa hali hiyo situ inakwamisha utendaji kazi bali inachangia hasara
kwa Mamlaka kwani hulazimika kutumia gharama kubwa kwaajili ya uwendeshaji
kifaa cha kukodisha.
Hata hivyo
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mwantumu Mahiza alisema kuwa uwamuzi wa Rais ni kwa ajili
ya kuhakikisha maendeleo ya nchi yanapatikana kwa haraka na kwa kutumia
raslimali kwa uwangalifu.
Alisema kuwa
sambamba na hilo ilikuweza kuongeza ufanisi katika bandari ameahidi kuunda tume
itakayokuwa ikishughulika na kutatua kero mbalimbali zinazoikabili bandari hiyo
kwa lengo la kuongeza ufanisi .
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment