Baadhi ya
Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa ya Serikali toka kwa Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (hayupo pichani) juu ya Uamuzi wa
Serikali wa kulifuta Gazeti la MAWIO katika Daftari la Msajili wa Magazeti mara
alipokutana na waandishi hao 17 Januari 2016 katika Ukumbi wa Idara ya Habari
uliopo jijini Dar es Salaam.PICHA NA MICHUZI JR-MMG.
SERIKALI YALIFUTA GAZETI LA MAWIO.
Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kulifuta kutoka katika Daftari la
usajili wa magazeti, gazeti lijulikanalo kama “MAWIO”.
Amri ya
kulifuta Gazeti hilo imetolewa kwa Tangazo la Serikali Na. 55 lililotolewa tarehe
15 Januari, 2016. Uamuzi huo umetolewa kwa mjibu wa Sheria ya agazeti Sura ya 229, kifungu 25(1).
Hatua hii
pia inazuia gazeti la Mawio kuchapishwa katika njia nyingine yoyote ikiwa ni
pamoja na mitandao (Online publication) kwa mujibu wa Sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki
na Posta Sura ya 306.
Serikali kwa
masikitiko makubwa, imechukua uamuzi huu kutokana na mwenendo wa uandishi wa gazeti
hilo usioridhisha wa kuandika na kuchapisha habari zenye mwelekeo wa uchochezi
na kuhatarisha amani, utulivu na usalama wa nchi yetu.
Aidha, hatua
hii ya kulifuta gazeti hilo imechukuliwa baada ya Msajili wa Magazeti kufanya
juhudi kubwa za muda mrefu kuanzia Juni, 2013 hadi Januari, 2016
kumtaka Mhariri wa gazeti hilo kubadili aina ya uandishi wa habari na
makala katika gazeti lake, bila mafanikio.
Msajili wa
magazeti kwa juhudi zake alifanya mawasiliano na mhariri wa gazeti hilo mara
nane kwa lengo la kutaka afanye marekebisho ya
mtindo wa kutoa habari zake lakini mhariri wa gazeti hilo hakuzingatia
ushauri mzuri aliopewa na Msajili wa Magazeti.
Ninatoa wito
kwa wamiliki, wahariri, waandishi na watangazaji wa habari kuzingatia sheria,Kanuni
na taratibu za taaluma ya uandishi wa habari ambazo zikizingatiwa hakutakuwa na
migogoro yoyote.
Aidha Serikali inasisitiza kwamba inaheshimu uhuru wa vyombo
vya habari unaozingatia maadili, weledi na Sheria za nchi na kwamba Serikali
itaendelea kushirikiana navyo.
Kwa upande
mwingine ninatoa pongezi kwa vyombo vyote vya habari nchini vinavyozingatia
maadili, weledi na Sheria zinazosimamia taaluma ya habari na sheria nyingine za
nchi.
Kwa namna ya
pekee Serikali inawapongeza wamiliki na wahariri wa vyombo vya habari ambavyo
vinapofanya makosa vikielekezwa hujirekebisha na kutoa ushirikiano kwa Serikali
na pia kubadili mwenendo wao; hawa ni pamoja
na wahariri wa magazeti ya;-
- Magazeti ya
Daily News na Habari Leo
Ninapenda kusisitiza kwamba Serikali inapenda kujenga uhusiano
mzuri na wa kirafiki kati yake na wadau wa sekta ya habari. Aidha ninasisitiza tena
wadau wa sekta hii kuzingatia Sheria ili kujenga heshima ya tasnia ya habari na
kulinda amani ya nchi yetu.
Imetolewa na Nape M. Nnauye(Mb,)
Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Dar es
Salaam, leo tarehe 17
Januari,
2016
|
No comments:
Post a Comment