Mamlaka ya
mawasiliano nchini Tanzania, TCRA imevifungia vituo 21 vya Radio na 6 vya
Television kwa muda wa miezi 3 kikiwemo kituo cha Star TV, Radio free Afrika,
Kiss Fm na Uhuru FM.
Vituo hivyo
vimefungiwa kutoa huduma kwa miezi mitatu kila moja baada ya kushindwa kulipa
kodi.
Kulingana na
mtandao wa jamii Forum,mnamo mwezi July 2015 Serikali ilitoa taarifa kwa umma
na TCRA kwamba baadhi ya radio na Televisheni zipatazo 40 zinadaiwa ada na tozo
mbalimbali.
Aidha
Serikali iliviagiza vituo hivyo kuhakikisha kuwa vimelipa ada kufikia tarehe 31
mwezi Disemba 2015.
Hatahivyo
baadhi ya vituo hivyo vililipa kodi hiyo mwanzoni mwa mwezi huu na wengine
wakishindwa kulipa.
Kwa mujibu
wa sheria unaposhindwa kulipa kodi TCRA huchukulia kwamba haupo.
TCRA sasa
inasema kuwa iwapo miezi mitatu ijayo itakamilika bila malipo hayo kufanywa
basi italazimika kuchukua hatua zaidi kama vile kuwapokonya leseni wahusika.
Ni vituo
11pekee kati ya vituo vilivyokuwa vikidaiwa na mamlaka hiyo vilivyotiii agizo
hilo na kulipa.
Baadhi ya
vituo hivyo ambavyo havitakuwa hewani kufikia jumatatu,January 18, 2016 ni
1. Sibuka FM
2. Breez FM
3. Country FM
4. Ebony FM
5. Hot FM
6. Impact FM
7. Iringa
Municipal TV
8. Kiss FM
9. Kitulo FM
10. Kifimbo FM
11. Mbeya City Municipal TV
12. Radio 5
13. Radio Free Afrika (RFA)
14. Musa Television Network
15. Pride
FM radio
16. Radio Huruma
17. Radio Uhuru
18. Star TV
19. Rock FM Radio
20.
Standard FM radio
21. Sumbawanga Municipal TV
22. Tanga City TV
23. Top Radio
FM limited
24. Ulanga FM
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii,
Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha
kwa WhatsApp +255789925630 .
|
No comments:
Post a Comment