VPL 2015/2016:-Ufahamu Msimamo wa Ligi Kuu baada ya Yanga SC kushinda bao 1 - 0 leo January 17,2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, January 17, 2016

VPL 2015/2016:-Ufahamu Msimamo wa Ligi Kuu baada ya Yanga SC kushinda bao 1 - 0 leo January 17,2016.

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Tanzania bara,Yanga SC imefanikiwa kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2015/2016 kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara jioni ya leo January 17, 2016,Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kikosi cha Yanga SC kilichoifunga Ndanda FC 1-0 leo Uwanja wa Taifa.

Bao hilo pekee, limefungwa na mfungaji Kevin Patrick Yondan kwa mkwaju wa penalti kipindi cha pili na sasa Yanga SC inafikisha pointi 36 baada ya kucheza mechi 14, ikilingana na Azam FC wanaoangukia nafasi ya pili.

Yanga SC sasa wanakaa kileleni mwa Ligi Kuu kwa wastani wa mabao tu, wakiwa wamefunga mabao 31 na kufungwa matano, wakati Azam FC imefunga mabao 28 na kufungwa tisa huku Simba SC inafikisha pointi 30 baada ya kucheza mechi 14, ikiendelea kukaa nafasi ya tatu.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630 .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad