LIGI KUU VODACOM 2015/2016:-Simba SC na ushindi ,Azam FC sare..Yanga SC leo kuongoza Ligi?? - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, January 17, 2016

LIGI KUU VODACOM 2015/2016:-Simba SC na ushindi ,Azam FC sare..Yanga SC leo kuongoza Ligi??

Wachezaji wa Simba Ibrahim Ajib (kushoto), Amis Kiiza (katikati) na Peter Mwalyanzi (kulia) wakishangilia goli lililofungwa na Amis Kiiza
Wachezaji wa Simba Ibrahim Ajib (kushoto), Amis Kiiza (katikati) na Peter Mwalyanzi (kulia) wakishangilia goli lililofungwa na Amis Kiiza.

Kocha wa Simba SC,Mganda Jackson Mayanja ameanza vizuri kibarua chake baada ya Jana January 16,2016, kukiongoza kikosi cha ‘wekundu wa Msimbazi’ Simba SC kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mechi yake ya  kwanza ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2015/2016 akiwa kama kocha wa timu hiyo  ambayo siku chache zilizopita imemfukuza aliyekuwa kocha wake mkuu Dylan Kerr.

Goli la Simba SC limefungwa na Amis Kiiza katika dakika ya nane kipindi cha kwanza bao ambalo limedumu hadi dakika ya 90 ya mchezo na kuishuhudia Simba ikiondoka uwanjani na pointi tatu mbele ya Mtibwa.

Ajib-baba Ubaya 1
Huko Azam Complex, Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, Azam FC walibanwa mbavu na kutoka Sare ya na African Sports ya Tanga katika Mechi ya Ligi Kuu Vodacom, VPL 2015/2016.

Sare hii imetoa mwanya mkubwa kwa leo Mabingwa Watetezi Yanga SC kutwaa uongozi wa VPL ikiwa wataifunga Ndanda FC kwenye Mechi itakayochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Azam FC sasa wamecheza Mechi 14 na wana Pointi 36 wakati Yanga SC wana Pointi 33 kwa Mechi 13 lakini wako bora katika Magoli.

Kwenye Mechi yao, Azam FC ndio walitangulia kwa Bao la Dakika ya 28 la Frank Domayo na Sports kusawazisha Dakika ya 59 kupitia Hamad Mbumba.
 
Matokeo ya michezo mingine iliyopigwa jana January 16,2016 kwenye viwanja vingine ni kama ifuatavyo:

JKT Ruvu 1 – 5 Mgambo JKT

Toto Africans 0-1 Tanzania Prisons

Stand United 1-0 Kagera Sugar

Mbeya City 1-0 Mwadui FC

Coastal Union 1-1 Maji Maji FC

Ajib-baba Ubaya
LIGI KUU VODACOM TANZANIA BARA 2015/2016.

Msimamo-Timu za Juu.

NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Azam FC
14
11
3
0
28
9
19
36
2
Yanga
13
10
3
0
30
5
25
33
3
Simba
14
9
3
2
21
9
12
30
4
Mtibwa Sugar
14
8
3
3
17
9
8
27

Ratiba

Jumapili Januari 17,2016.

Yanga SC v Ndanda FC

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630 .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad