(KUMRADHI KWA PICHA):-Msaada wa Wasamaria wema wa Matibabu Unahitajika kwa Kaka huyu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, January 17, 2016

(KUMRADHI KWA PICHA):-Msaada wa Wasamaria wema wa Matibabu Unahitajika kwa Kaka huyu.


Bw Antony Eustace Mkazi wa Kijiji  cha Bushangaro kata Nyakakika wilaya ya  Karagwe mkoani Kagera anayesumbuliwa  na  tumbo baada ya kufanyiwa upasuaji  kwa kuamisha sehemu ya haja kubwa na kuiweka pembeni mwa tumbo,anaomba  msaada wa shilingi laki saba ili apatiwe matibabu katika hospital ya rufaa ya Bugando iliyopo Jijin Mwanza.

Bw Antony amesema kuwa mwaka 2014 alipata matatizo ndani ya tumbo na baada ya kwenda hospitali ya Nyakahanga iliyopo wilayani Karagwe,Madakitari walilazimika kuhamisha sehemu ya haja kubwa na kuiweka pembeni mwa tumbo ili waweze kutibu sehemu iliyokuwa na tatizo.

Baada ya Muda wa miezi sita tangu Bw.Antony afanyiwe upasuaji, alirudi katika hospitali ya Nyakahanga na kuambiwa  madakitali waliomfanyia upasuaji walishaondoka hospitalini hapo na kumrufaa katika hospitali ya Bugando ambapo kuna madakitari wa kuweza kurudisha sehemu ya haja kubwa katika sehemu yake.

Bw Antony baada ya kufika katika hospitali ya Bugando ambapo aliambiwa alipe  kiasi cha fedha  shilingi laki saba ili kuweza kurudisha sehemu ya haja kubwa katika sehemu yake.

Kwa yeyote atakaye guswa anaweza kuwasiliana na  Bw. Antony Eustace AU KUMTUMIA MCHANGO WAKO KUPITIA NAMBA +255743022789 / +255789627789…. KUTOA NI MOYO.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630 .


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad