AJALI / PICHA:- Watu 3 wamefariki na 35 kujeruhiwa katika jali ya basi mkoani Morogoro. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, January 17, 2016

AJALI / PICHA:- Watu 3 wamefariki na 35 kujeruhiwa katika jali ya basi mkoani Morogoro.

Watu watatu wamefaiki dunia na wengine 35 kujeruhiwa vibaya katika ajali ya gari iliyohusisha basi la Kiruto Express likitokea Kondoa kwenda Dar es Salaam wakati dereva wa basi la Site Boy kutaka kulipita gari lingine bila tahadhari katika eneo la Kiegeya wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.

Wakizungumza na Wana Habari, mashuhuda wa ajali hiyo akiwemo kondakta wa basi lililopata ajali wamesema ajali hiyo imetokea majira ya saa sita mchana,Jana January 16,2016 wakati basi hilo likitokea wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma ambapo wameeleza ajali hiyo ilivyotokea.

Majeruhi wa ajali hiyo wanatibiwa  katika hospitali ya misheni ya Berega ambapo mganga mkuu wa hospitali hiyo Dokta Bahati Chiponda amekiri kupokea mili miwili na majeruhi 35 na kwamba majeruhi mmoja amefariki wakati akipatiwa matibabu na kupelekea idadi ya waliopoteza maisha kufikia watatu.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad