![]() |
Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara , VPL
– 2015/2016, kesho Jumamosi December 12 na 13,2015 inarejea kwa kishindo kwa
mitanange mikali ikiwepo ile Mechi ya mvuto mkubwa kati ya Vinara wa Ligi Azam
FC na Simba SC huku Mabingwa Watetezi Yanga SC wakiwa Mkwakwani, Tanga kucheza
na Mgambo JKT wakati Jumapili Uwanjani hapo hapo ipo Dabi ya Tanga kati ya
Coastal Union na African Sports.
Baada ya Mechi 9 Azam FC wapo juu
kwenye VPL wakiwa na Pointi 25 wakifuatiwa na Mabingwa Watetezi Yanga SC wenye
Pointi 23 kisha Mtibwa Sugar Pointi 22 na Simba SC wapo Nafasi ya 4 wakiwa na
Pointi 21.
Kwenye Mechi za Wikiendi hii, huenda
baadhi ya Timu zikawa zina Wachezaji wapya baada ya kuimarisha Vikosi vyao kwa
kutumia Dirisho la Uhamisho la Kipindi hiki.
Simba SC wao wamemrejesha Straika
kutoka Kenya, Paul Kiongera, na pia kuwanunua Beki wa African Sports, Novat
Makunga, na Straika wa Mtibwa Sugar Haji Ugando.
Azam FC wao wamemchukua Kipa Ivo
Mapunda ambae alizidakia Klabu kubwa hapa Nchini nan je ya Nchi alipokuwa na
Gor Mahia ya Kenya na Saint George ya Ethiopia.
LIGI KUU VODACOM 2015/2016 -RATIBA
Jumamosi Desemba 12,2015.
Kagera Sugar v Ndanda FC
Stand United v Mwadui FC
Mbeya City v Mtibwa Sugar
Azam FC v Simba SC
Majimaji v Toto Africans
Mgambo JKT v Yanga SC
Jumapili Desemba 13,2015.
JKT Ruvu v Tanzania Prisons
Coastal Union v African Sports
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp . |
Post Top Ad
Friday, December 11, 2015

VPL – 2015/2016:-Azam FC v Simba SC na Mgambo JKT v Yanga SC kesho December 12,2015.
Tags
# MICHEZO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
Makala Inayofuata
VPL 2015/2016:-Tazama Matokeo yote ya Ligi Kuu Bara leo hii December 12,2015.
Makala Iliyopita
MUHIMU SANA:-Namba za Simu za Kuripoti Kero TRA na taarifa za siri za Watumishi Wabadhirifu.
Luka Modric Mchezaji Bora Ulaya 2017/2018, Ronaldo Mshambuliaji Bora.
AnonymousAug 31, 2018Azam na Yanga zaibuka na Ushindi Ligi Kuu Tanzania Bara.
AnonymousAug 24, 2018Shule 18 za Sekondari Ngara zapokea Vifaa vya Michezo kutoka Coca Cola.
AnonymousAug 03, 2018
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment