Mkuu wa
Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma,SSP Nuru Selemani
akiwakiwaelimisha abiria ndani ya basi lilofanya safari zake mikoani ikiwa ni
sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya”Wait to Send”inayotoa elimu kwa madereva
kutokutumia simu na kilevi wakati wote wakitumia vyombo vya moto.Kampeni hiyo
inadhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Kaimu mkuu
wa kanda ya kati wa Vodacom Tanzania,Heladius Kisiwani(kulia)akimpa maelezo
dereva wa basi liendalo mikoani,Masoud Selemani kuhusiana na pete ya kidoleni
inayotolewa na Kampuni hiyo kwa kushirikiana na jeshi la Polisi kitengo cha
Usalama barabarani yenye ujumbe“Wait To Send” unaohamasisha madereva wa vyombo
vya moto kutokutumia simu za mkononi wakiwa wanaendesha vyombo hivyo. Zoezi
hili lilifanyika leo katika kituo cha mabasi yaendayo mkoani cha
Dodoma.
Katikati Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma,SSP Nuru
Selemani.
Mkuu wa
kitengo cha elimu kwa Umma kitengo cha Usalama barabarani makao makuu ya Polisi
ASP,Abel Swai akitoa elimu kwa abiria ndani ya basi liliendalo mikoani katika
stendi kuu ya mabasi Dodoma ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya”Wait to
Send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote
wakitumia vyombo vya moto.Kampeni hiyo inadhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Mkuu wa
Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma,SSP Nuru Selemani(kulia) akitoa
maelezo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)Kuhusiana na mwendelezo wa
kampeni ya”Wait to Send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi
wakati wote wakitumia vyombo vya moto.Kampeni hiyo inadhaminiwa na Vodacom
Tanzania.
Wengine kutoka kusho ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu
na Kaimu Mkuu wa kanda ya kati wa kampuni hiyo Heladius Kisiwani.
Shughuli
ikiendelea ya kutoa elimu kuhusiana na mwendelezo wa kampeni ya”Wait to
Send”inayotoa elimu kwa madereva kutokutumia simu na kilevi wakati wote
wakitumia vyombo vya moto.
Kampeni hiyo inaendeshwa na Jeshi la polisi la
Usalama barabarani kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania.
Kampeni ya
usalama barabarani ya kuwataka madereva nchini kuzingatia sheria za usalama
barabarani,December 22,2015 imefanyika katika Mkoa wa Dodoma.
Madereva
wameendelea kuhimizwa kutotumia vinywaji vyenye ulevi na kuacha tabia ya
kuongea na simu au kutuma na kupokea ujumbe wa maneno (sms) wanapokuwa
wanaendesha vyombo vya moto.
Mkuu wa
kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Dodoma, SSP Nuru Selemani amesema kampeni
hii ni muhimu katika kupunguza matukio ya ajali “Watumiaji wa barabara hii ya
mkoa wa Dodoma ni wengi hususani madereva wa vyombo vya moto hawana budi
kuzingatia maelekezo ambayo tumekuwa tukiwapa katika kampeni hizi ili tupate
matokeo mazuri kwa kupunguza ajali kama ilivyokusudiwa”Alisema
Alisema
madereva wakizingatia sheria za barabarani kwa kiasi kikubwa ajali
zinazoendelea kutokea kila siku zitapungua hususani katika kipindi hiki cha
msimu unakoelekea wa sikukuu na aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa kuunga mkono
jitihada za serikali katika kupambana na tatizo hili ambalo limekuwa sugu .
Kwa upande
wake,Kaimu Mkuu wa kanda ya kati wa asoko wa Vodacom Tanzania Heladius
Kisiwani, alisema Vodacom itaendelea kushirikiana na serikali katika kuunga
mkono jitihada za kuondoa matatizo kwenye jamii kama lilivyo tatizo hili la
ajali ili kuhakikisha wananchi wanaishi maisha murua na marefu.”Tunatoa rai kwa
madereva wote kuzingatia sheria za barabarani na kutokutumia simu wakati wowote
wakiwa wanatumia vyombo vya moto”.
Aliongeza
kuwa Vodacom itakuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii athari za kuendesha gari
wakati huo huo unatumia simu ya mkononi kupitia kampeni ya “Wait to Send” pia
itaendelea kuhamasisha madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Alisema
kampuni hiyo itaendeleza kutoa elimu kwa mikoa mingine pia katika uhamasishaji
wa madereva kuzingatia sheria za barabarani katika miji ya Morogoro,Dar es
Salaam na mikoa mingine na kampeni hizi zitaendelea kufanyika sehemu mbalimbali
nchini.
Katika
kampeni ya leo wafanyakazi wa Vodacom kwa kushirikiana na askari wa usalama
barabarani walitoa uhamasishaji kwa madereva kuacha kuongea na simu
wanapoendesha vyombo vya moto na kuwagawia madereva pete maalum za
kuwatahadharisha kutotuma ujumbe wa simu za mkononi wanapokuwa wanaendesha
vyombo vya moto pia zoezi la kupima madereva kubaini kama wanatumia vilevi
lilifanyika ambapo wadereva waliokutwa wanaendesha vyombo vya moto
walichukuliwa hatua kali za kisheria.
Baadhi ya
abiria walioshuhudia kampeni hii mkoani Dodoma wamesema ni ya muhimu itasaidia
kupunguza ajali nchini.”Hivi sasa ajali nyingi zinazotokea hapa nchini
zinasababishwa na uzembe wa madereva,kampeni hizi zikiendelea zitapunguza ajali
kwa kiasi kikubwa”.Alisema Sunday Israel mkazi wa Dodoma aliyekuwa safarini
kuelekea Singida.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
|
No comments:
Post a Comment