Ponnar, kijana aliyefanyiwa
upandikizaji wa Moyo na Ini kwa pamoja, katika hospitali ya Apollo akizungumza
na waandishi wa habari baada ya upandikizaji huo.
Na Mwandishi
Wetu,
Hospitali za Apollo zimefanikiwa
kwa mara ya kwanza barani Asia kufanya upandikizaji wa moyo na ini; hivyo
kujiunga na timu ya hospitali chache duniani zilizowahi kufanya upasuaji huo wa
aina yake.
Desemba 2015; Hospitali za Apollo
ambazo ni kinara barani Asia kwa ubora wa huduma za afya, kwa mara nyingine
zimeonyesha ubora wake wa uongozaji kupitia kituo cha upandikizaji duniani kwa
kufanikisha upasuaji wa upandikizaji kwa mpigo wa ogani za moyo na ini
kwa kijana mwenye umri wa miaka 30 anayetokea Tiruchengode,
Tamilnadu nchini India.
Tukio hilo linalotambulika kitaalam kama en-Bloc
CHLTni mfumo mgumu wa upasuaji na haujawahi fanyika popote barani Asia.
Kama ilivyoitwa na chuo cha Stanford kuwa ni “upasuaji wa kiufundi na kitaalam
sana, ambao ni vyema uachwe kwenye mikono ya madaktari bingwa wenye ujuzi”, ni
hizo hatua za CHLT pekee zimeweza kufanyika ulimwenguni pekee.
Stori hii
ya Ndg. Ponnar, kijana mtulivu kutokea Tiruchengode, mji mdogo kutokea wilaya
ya Namakkal Tamilnadunchini India. Ponnar alikuwa ni mwanafunzi bora
aliyemaliza stashahada yake kwenye fani ya uhandisi na alikuwa na medali ya
dhahabu.
Katika umri wa miaka 22, kama kijana mwenye malengo makubwa na matumaini
ya kufikia ndoto zake, Ponnar alianza kuhisi kujaa maji tumboni mwake, upungufu
wa pumzi na kujikuta rangi ya ngozi yake kuanza kuwa manjano.
Hii
ilitambulika kama kufeli kwa ini, iliyopelekea kufanyiwa kwa upandikizaji wa
ini, ambao familia yake ilikuwa tayari kwa kijana huyo kufanyiwa hilo zoezi la
upandikizwaji.
Wakati alipofika kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji huo wa
kupandikizwa ini, iligundulika kuwa Ponnar anatatizo katika mfumo wa upumuaji
unaoitwa kitaalam Ebsteins anomaly au kufeli kwa upande wa
kulia wa moyo katika kufanya kazi kwa usahihi ambao ndio awali umeletea udhoofu
katika ini.
Bahati
mbaya kujumuika kwa matatizo mawili kwa mpigo kulimfanya Ndg Ponnar kutokuwa na
njia mbadala yoyote mbali na kujumlisha upandikizaji wa ini na moyo.
Hii
ni hatua ya upasuaji inayohusisha njia kuu mbili kwanza ya kupitia kooni
na kifuani (kwa ajili ya moyo) na kupitia tumboni (kwa ajili ya ini) hivyo
kufanya zoezi kuwa hatari sana.
Ponnar- kwa
utulivu na ukakamavu alijiandaa kupigania uhai wake mpaka mwisho.
Familia yake
hasa dada yake ambaye alikuwa tumaini na nguzo kwake, maamuzi ya kwamba
watafanya lolote liwezekanalo kuhakikisha wanamwokoa kijana wao,
walimpelekea hospitali za Apollo, Chennai, India.
“kwa tatizo
la kuwa na moyo usiofanya kazi ipasavyo, kulikuwa na presha kubwa upande wa
nyuma wa ini iliyosababisha kuharikika kwa seli za ini iliyopelekea udhoofu huo
wa ini. Kwa kuongezea, timu ya upandikizaji wa ogani walijadili uwezekano
mkubwa wa uvujaji mwingi wa damu hasa kwa kuwa ni upasuaji wa sehemu mbili kwa
mpigo na pia uwezekano mkubwa wa sumu kujikusanya kwenye ini, kuathiri moyo
hasa kama ogani hizo mbili zitapandikizwa tofauti tofauti” alisema ”Dk. Paul
Ramesh, mshauri mwandamizi wa upasuaji katika mfumo wa upumuaji kutoka
hospitali za Apollo, Chennai.
Upasuaji na
upandikizaji wa moyo na ini unaweza fanyika kwa njia kuu tatu;-
1. Kwanza upandikizaji wa moyo- ufuatiwe na upandikizwaji
wa ini pale mgonjwa atapokuwa amepata nafuu kutokana na upasuaji wa kwanza.
2. Kwanza upandikizwaji wa moyo- ufuatiwe na
upandikizwaji wa ini kama njia mbili tofauti ila kwa mpigo katika operesheni
moja.
3. Upandikizwaji wa moyo na ini kwa pamoja, inafanyika
kwa ogani zote kuchukuliwa kama moja na kupachikwa kwa pamoja kwa mpigo.
Ni wale
mabigwa tu kwenye ile timu ya upandikizwaji wa ogani kufanya kazi pamoja kama
timu moja na kuleta matumaini ya kufanikisha en-bloc CHLT mfumo
adimu sana kufanyika duniani.
”kwa zaidi
ya miongo ya ujuzi katika upandikizwaji wa ogani, imetuwezesha kupata maarifa
na utaalamu unaohitajika kufanya operesheni ngumu kama hizi. Mafanikio
yetu katika upandikizwaji wa moyo na ini yaliyopatikana yametupatia msingi na
uimara katika uendeshaji bora wa en-bloc CHLT kwa bara la
Asia.
Najivunia sana kwa ajili ya Ponnar na familia yake walioweza kuimanini
timu kutoka hospitali yetu ya Apollo, imetupa sana motisha sisi kuendelea mbele
na mfumo huu bila mipaka ili kufika juu kabisa. Aliongeza Dk. Ramesh.
Ponnar
alisubiri kutokea April hadi 0ktoba 2015 ili mtoaji damu anayemfaa
alipopatikana. Alifanyiwa upasuaji wa upandikizwaji huo wa moyo na ini tarehe
14 oktoba 2015 na aliruhusiwa kwenda nyumbani ndani ya wiki baada ya upasuaji
huo.
Leo hii, Ponnar ni mzima wa afya njiani kuelekea kupona kabisa na kurudia
maisha yake ya awali- ni mwenye furaha sababu ngozi yake sio ya njano tena, na
sasa anaweza kuendelea kufurahia raha za maisha kama kutembea kwa miguu yake
mwenyewe.
Kwa maumivu yaliyokuwa nyuma kwa miaka 8, sasa Ponnar yupo huru
kuendeleza matumaini yake na ndoto zake.
Ngazi hii
ya kimatibabu, ya upandikizwaji wa moyo na ini kwa mpigo (mara ya kwanza barani
Asia) ni hazina kubwa kwa Ndg Ponnar na dada yake,walioweza kutosikiliza uzushi
wa watu wote.
Pia ni ushuhuda kuwa timu ya madaktari wa upandikizwaji kutoka
hospitali za Apollo Chennai wamefanikiwa kufanya operesheni hii kwa mafanikio
makubwa.
Haya yote yasingeweza kufanikiwa kama pia kusingekuwepo kwa
ushirikiano mkubwa kutoka serikali ya Tamilnadu na programu ya kujitolea ogani
iliyopo Tamilnadu ambayo imesifiwa ulimwenguni kwote kwa kazi kubwa
walioifanya.
”mafaniko
haya makubwa ni agano kwa mabingwa wote wa upasuaji duniani, madaktari,
wataalam, manesi na wafanyakazi wote waliojitolea kuwahudumia wagonjwa na kutoa
huduma zilizopo katika viwango vya kimataifa.
Upasuaji ni matokeao ya mipango
bora iliyofanywa kwa siku kadhaa kutoka kwa timu ya wataalam upande wa moyo na
ini na uonekanaji wa miundo mbinu bora na wataalam waliokubuhu.
Jitihada hizi
shirikishi zinachukua timu zote za upandikizaji ili kutathimini na kuweka
mikakati kasha kuonyesha kuwa fani hii ni ya kuheshimika”. Alisema Dk.
Prathap C Reddy, mwenyekiti na mwanzilishi wa Hospitali za Apollo
Kuhusu Hospitali za Apollo
Hospitali ya Apollo ilifunguliwa
mnamo mwaka 1983, na kutoka kipindi hicho imekuwa ikiendeshwa kwa kauli mbiu
isemayo "Dhamira yetu ni kuleta huduma ya kisasa karibu kabisa na
walengwa. Tunajitolea kutoa huduma bora na mafanikio katika elimu na
utafiti kwa ajili ya jamii ya kibinadamu".
Katika
miaka 30 tokea kuanzishwa kwake, hospitali ya Apollo imeandika historia
kubwa kupata kuonekana nchini India. Ni moja ya kampuni kubwa ya Afya katika
bara la Asia, na pia imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya afya nchini
india.
Katika safari yake, imeweza kuboresha maisha ya watu wapatao
milioni 39 kutoka nchi 120.Inatoa huduma maalum 52 na vitanda vya upasuaji
710.Imefanya upasuaji wa moyo wenye kufikia idadi ya watu 152,000 na panuzi
125, 000 za mishipa myembamba.
Imefanya upasuaji wa wa viungo unaopita kiasi cha
idadi ya watu 10,000, upasuaji wa uvimbe wa ubongo, uti wa mgongo na
zaidi.
Taasisi ya Apollo ni moja ya taasisi zinazoongoza nchini india, zikiwa na
teknolojia za kisasa kama Novalis TX, PET MRI na Upasuaji unaotumia mashine za
kiroboti.
Waambie Wenzako!
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .
|
No comments:
Post a Comment