Muonekano wa
Moto mkali ukiunguza Ofisi za Kliniki ya afya ya Mapenzi iliyopo jijini Mwanza.
Na Idd
Mumba, Mwanza
Ofisi za
Kliniki ya afya ya Mapenzi iliyopo jijini Mwanza karibu na jengo la Nyanza jana
December 22,2015, majira ya saa tisa alasiri imeungua moto na kuteketeza vitu
mbalimbali vilivyokuwepo katika kliniki hiyo.
Wakizungumza
na www.globalpublishers.co.tz mashuhuda wa tukio hilo wamesema waliona moshi
ukitoka katika ofisi hizo na kutoa taarifa kwa jeshi la zimamoto ambalo
liliwahi kufika katika eneo la tukio lakini walitumia muda mrefu kufunga bomba
la kurushia maji jambo lililosababisha kuungua kwa vifaa vingi vya ofisi hiyo.
Kwa upande
wake, mmiliki wa kliniki hiyo, Paul Nelson amesema wakati tukio hilo linatokea
yeye alikuwa Mwanza Hotel iliyopo karibu na ofisi hiyo na aliona moshi mkubwa
ukitoka katika ofisi yake na kutoa taarifa kwa zimamoto.
Nelson
amesema chanzo cha moto huo kimenatokana na shoti ya jenereta lililokuwa
limewashwa kutokana na kukatika kwa umeme na jenereta hilo lilikuwa halitumiki
kwa muda mrefu jambo ambalo limefanya kutokea kwa shoti hiyo na kusababisha
moto mkali uliounguza ofisi yake.
Alivitaja
vifaa vilivyoungua kuwa ni pamoja na laptop yenye thamani ya shilingi laki nane
(800,000/=), simu mbili pamoja na mafaili aliyokuwa anayatumia katika ofisi
hiyo.
|
Ofisi hizo
zikizidi kuungua kwa moto.
|
Zimamoto
wakijaribu kupambana na moto huo.
|
No comments:
Post a Comment