UWEKEZAJI/PICHA:-Rais Kikwete azindua Kiwanda cha Saruji cha DANGOTE Mtwara. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, October 12, 2015

UWEKEZAJI/PICHA:-Rais Kikwete azindua Kiwanda cha Saruji cha DANGOTE Mtwara.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  Alhaj Aliko Dangote wakifunua pazia kuashiria  kuzindua rasmi kiwanda cha saruji cha Dangote ambacho ni kikubwa kuliko viwanda vyote vya saruji Afrika Mashariki huko Mtwara Jumamosi Oktoba 10, 2015.

Inaelezwa kuwa Kiwanda hicho kitatoa ajira 1,500 za moja kwa moja sambamba na vibarua 9,000.

 Kwenye list ya Matajiri wakubwa wanaotambulika Duniani kwa sasa yuko pia mfanyabiashara Alhaji Aliko Dangote ambaye ni Raia wa Nigeria, Afrika anatajwa kuwa tajiri wa kwanza kabisa.

Utajiri wake unatokana na nguvu kubwa ambayo amewekeza kwenye Biashara na Miradi mbalimbali ikiwemo Miradi ya Sukari, Cement, Mafuta na Biashara nyingine kubwakubwa.

Alikuja Tanzania pia akahitaji kuwekeza moja ya Miradi yake mikubwa, akapata ruhusa ya kufanya ujenzi wa Kiwanda cha Cement Mtwara.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  Alhaj Aliko Dangote na ujumbe wake kutoka Nigeria wakipata picha ya kumbukumbu wakati wa sherehe za kuzindua kiwanda hicho kikubwa kuliko viwanda vyote vya saruji Afrika Mashariki huko Mtwara Jumamosi Oktoba 10, 2015.



d3

d22
Alhaji Aliko Dangote kwenye Hotuba.

d25

d29
Rais Kikwete kwenye Hotuba pia ya Uzinduzi.

d35
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na  Alhaj Aliko Dangote na familia yake na ujumbe wake kutoka Nigeria wakipata picha ya kumbukumbu wakati wa sherehe za kuzindua kiwanda hicho kikubwa kuliko viwanda vyote vya saruji Afrika Mashariki huko Mtwara Jumamosi Oktoba 10, 2015.

d37
Sehemu ya wafanyakazi wa kiwanda kipya cha Saruji cha Dangote Alhaj Aliko Dangote  wakati wa sherehe za kuzindua kiwanda hicho kikubwa kuliko viwanda vyote vya saruji Afrika Mashariki huko Mtwara Jumamosi Oktoba 10, 2015.

d41
Muonekano wa moja ya sehemu za ndani ya Kiwanda.

d45
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad