KOMBE LA DUNIA 2018:-Taifa Stars kuivaa sasa Algeria. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, October 12, 2015

KOMBE LA DUNIA 2018:-Taifa Stars kuivaa sasa Algeria.

Mshambuliaji wa Tanzania, Mbwana Samatta akiwatoka wachezaji wa Malawi katika mchezo wa marudiano hatua ya kwanza ya mchujo wa kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania kucheza Kombe la Dunia mwaka 2018 jana October 11,2015,Uwanja wa Kamuzu, Blantyre. Malawi ilishinda 1-0 lakini Tanzania imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-1 baada ya awali kushinda 2-0 Dar es Salaam..picha zote kwa hisani ya Binzubeiry.co.tz.
Thomas Ulimwengu wa Tanzania akiambaa na mpira dhidi ya wachezaji wa Malawi Hapo jana .



Beki wa Tanzania, Mwinyi Mngwali akiruka na Gerald Phiri wa Malawi kuwania mpira wa juu.
Mshambuliaji wa Tanzania, John Bocco akiambaa na mpira katikati ya wachezaji wenzake.

Timu ya Taifa ya Tanzania hapo jana October 11,2015 imefungwa Bao 1-0 huko Uwanja wa Kamuzu Banda, Blantyre na Wenyeji Malawi katika Mechi Marudiano ya Raundi ya Kwanza ya Kanda ya Afrika ya Mchujo wa Kombe la Dunia ambazo Fainali zake zitafanyika huko Russia Mwaka 2018 lakini imesonga Raundi ya Pili kwa Jumla ya Bao 2-1 katika Mechi mbili.

Katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa Jumatano iliyopita Tanzania iliichapa Malawi 2-0 kwa Bao za Maprofeshanali Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ambao wote hucheza huko Congo DR kwenye Klabu ya Lubumbashi TP Mazembe.

Tanzania sasa watacheza Raundi ya Pili na Algeria ambao wanaanzia hatua hiyo ambayo Mechi zake zimepangwa kuchezwa Jijini Dar es Salaam Novemba 9 na Marudiano huko Algiers hapo Novemba 17,2015.

Washindi wa Raundi ya Pili wataingizwa kwenye Droo ya kupanga Makundi 5 ya Timu 4 kila mmoja ambapo Washindi wake wataenda Fainali Russia moja kwa moja.

Raundi ya Pili

**Mechi kuchezwa Novemba 9 hadi 17

Somalia/Niger v Cameroon

South Sudan/Mauritania v Tunisia

Gambia/Namibia v Guinea

Sao Tome/Ethiopia v Congo

Chad/Sierra Leone v Egypt

Comoros/Lesotho v Ghana

Djibouti/Swaziland v Nigeria

Eritrea/Botswana v Mali

Seychelles/Burundi v DR Congo

Liberia/Guinea Bissau v Ivory Coast

CAR/Madagascar v Senegal

Mauritius/Kenya v Cape Verde

Tanzania v Algeria

Sudan v Zambia

Libya v Rwanda

Morocco v Equatorial Guinea

Mozambique v Gabon

Benin v Burkina Faso

Togo v Uganda

Angola v South Africa

**Washindi kutinga hatua ya Makundi


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad