Pichani kushoto ni Mwenyekiti
wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.
Mwenyekiti
wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha ametangaza kufuta matokeo
ya Uchaguzi mkuu visiwani Zanzibar,
uliofanyika Oktoba 25, 2015.
Jecha
amesema kuwa, ZEC imefuta matokeo ya uchaguzi kutokana na kukiukwa kwa sheria
na taratibu mbalimbali za uchaguzi wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo.
Uchaguzi huo
utarudiwa baada ya siku 90.
Amesema
baadhi ya makamishna wa tume hiyo, badala ya kutekeleza majukumu yao inavyotakiwa
kikatiba "wamekuwa ni wawakilishi wa vyama vyao".
Tangazo la
mwenyekiti huyo limetolewa huku hali ya wasiwasi ikiendelea kutanda visiwani
humo.
Siku moja
baada ya uchaguzi kufanywa,October 26,2015 mgombea wa chama cha upinzani cha Civic United From
(CUF) Seif Sharif Hamad alijitangaza kuwa mshindi, hatua iliyokemewa na chama
cha CCM ambacho mgombea wake Dkt Ali Mohamed Shein amekuwa rais wa visiwa hivyo
muhula unaomalizika.
Tume ya
uchaguzi visiwani Zanzibar - ZEC pia ilishutumu hatua ya mgombea huyo.
Kabla ya
kufutiliwa mbali kwa matokeo ya uchaguzi, tume hiyo ya uchaguzi ilikuwa
imetangaza matokeo ya majimbo 31 kati ya majimbo 54 visiwani humo.
Hayo
yakijiri Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania - NEC inaendelea kutoa matokeo ya
uchaguzi wa URAIS. Kufikia sasa imetoa matokeo ya majimbo 155 kati ya majimbo
264.
TAARIFA
ZAIDI HAPA CHINI
|
No comments:
Post a Comment