Baada
ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, ZEC kutangaza
kufuta matokeo ya Uchaguzi mkuu wa Zanzibar October 28 2015, Kiongozi wa zamani
wa chama cha CUF, Professor Ibrahim Haruna
Lipumba na mgombea Urais wa Zanzibar kwa mwamvuli wa CUF na
Umoja wa vyama vya UKAWA, Maalim Seif Sharif
Hamad wamezungumzia kuhusu kuchukuliwa kwa hatua hiyo.
“Nimeshtushwa na hatua hiyo hasa ukizingatia Uchaguzi
umefanyika tarehe 25 leo ni tarehe 28, na sababu ambazo Mwenyekiti amezitoa ni
mambo ambayo yangeweza kujulikana mapema sana… Tume ya Uchaguzi ya Taifa ambayo
inatangaza matokeo ua Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa
inatangaza Kura za matokeo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ambazo zimefanyika
kwenye uchaguzi huohuo mmoja na Tume haijasema kwamba uchaguzi ule ulikuwa
mbovu.”- Professor Ibrahim Haruna Lipumba.
|
“Hata watazamaji
wa Kimataifa wamesema utaratibu wa kupiga Kura na kuhesabu vituoni ulikwenda
vizuri… nashukuru viongozi wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amewaomba
Wazanzibar kuwa watulivu wakati suala hili linashughulikiwa.” >>>
Prof. Lipumba.
|
“Ilipaswa iundwe Tume ya Majaji watazame tamko alilolitoa lina
uhalali gani, wazungumze pia na Wajumbe wa Tume ya uchaguzi kwa sababu tamko
hilo limevunja Sheria halina uhalali wa kisheria.”
Hili
ndio jibu la Professor Lipumba kuhusu anayeweza kumaliza
tatizo lililotokea Zanzibar >>> “Mtu
ambaye ana uwezo na wajibu mkubwa kwenye hili ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, kwa sababu yeye ni Rais na Mwenyekiti wa CCM, ashauriane na Rais wa
Zanzibar ili akubali kuunda Serikali ya kitaifa, imefika wakati Dk. Shein
aoneshe ukomavu wa kisiasa.”
|
“Kuna watu wamelalamika, nimemsikia Edward Lowassa
amelalamikia matokeo ya Uchaguzi, haya ambayo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi
Zanzibar ameyaeleza yanaongeza nguvu kwa Mheshimiwa Lowassa kwamba hata Tanzania bara mambo hayakwenda sawa… Hatua
aliyochukua Mwenyekiti imevunja Sheria, isipotokea ufumbuzi mapema, patatokea
vurugu.” >>> Professor Ibrahim Haruna
Lipumba.
HAPA
NAANZA NA KILE ALICHOKISEMA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD.
“Chama cha CUF kimepata taarifa kwamba Mwenyekiti wa Tume ya
uchaguzi Zanzibar ametangaza kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu bila
kuwashirikisha Makamishna wenzake wa Tume ya Uchaguzi…. CUF imeshtushwa na
taarifa hii ambayo iko kuinyume na Sheria za uchaguzi ya Zanzibar, Mwenyekiti
hana mamlaka ya kufuta Uchaguzi huo.” >>> Maalim Seif
Sharif Hamad.
|
“Mwenyekiti
hakutafakari kwamba kuufuta uchaguzi Zanzibar kunaathiri pia Uchaguzi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu wapiga Kura ni walewale waliomo
kwenye daftari la wapiga Kura wa ZEC.”
|
“Rais wa
Jamhuri ya Muungano hawezi kupatikana kwa kupigiwa Kura na wananchi wa Tanzania
bara pekeyake… Tunatambua kwamba hatua hii imekuja baada ya majaribio ya
kulazimisha ushindi kushindikana.”
|
“CUF
hatutambui uamuzi huo wa Mwenyekiti wa Tume ya ZEC, tunaitaka Serikali na CCM
kuiacha Tume iendelee na uhakiki wa matokeo na itangaze mshindi… Tunatoa wito
na kuomba Wazanzibar kwa ujumla kubaki watulivu..” >>> Seif Sharif
Hamad. Sauti yote ya Maalim Seif Sharif Hamad hii hapa kama umepitwa na hii taarifa.
|
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment