UCHAGUZI MKUU 2015 TANZANIA:-Matokeo Tazama kutoka Jimbo la Buyungu ,Muhambe,Kasulu na Biharamulo Magharibi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, October 27, 2015

UCHAGUZI MKUU 2015 TANZANIA:-Matokeo Tazama kutoka Jimbo la Buyungu ,Muhambe,Kasulu na Biharamulo Magharibi.


Bw Kasuku Bilago.

Jimbo la Buyungu / Kakonko: Mgombea ubunge wa Jimbo la Kakonko  kupitia CHADEMA, Bw Kasuku Bilago ameibuka mshindi katika jimbo hilo .

Bw Bilago ameshinda kwa jumla ya kura 23,041 dhidi ya mpinzani wake wa karibu ,Mhandisi Christopher Chiza  wa CCM aliyepata kura  22,984.

Wafuasi wa Bw Kasuku Bilago wakishangilia ushindi wake wa Jimbo la Buyungu/Kakonko.

Jimbo la Muhambwe /Kibondo: Mgombea Ubunge Jimbo la Muhambwe  kupitia chama cha Mapinduzi CCM ,Eng.A.J Nditiye  ameshinda ubunge wa jimbo hilo kwa kura 27,225,akimwangusha mpinzani wake Bw.Felix Mkosamali wa NCCR-Mageuzi aliyepata kura 21,630.

Jimbo la Kasulu Mjini: Mgombea ubunge Jimbo la Kasulu Mjini, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) ameshinda ubunge wa jimbo hilo kwa kura 25,336 na kufanikiwa kulirejesha jimbo hilo chama Tawala kwa kuwashinda wapinzani wake wa karibu ACT Wazalendo kura 22,512 na NCCR Mageuzi kura 3,488.

Jimbo la Kasulu Vijijini: Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo Bw.Philimon Magesa amemtangaza Bw.Augustino Vuma Hole wa  CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 36,940, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Bi. Agripina Buyogera wa NCCR Mageuzi, aliyekua akitetea jimbo hilo kwa kupata kura 19,941

Jimbo la Biharamulo Magharibi: Bw.Mukasa Oscar Rwegasira wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 41,879, dhidi ya mpinzani wake wa karibu  Dr Antony Gervas Mbasa wa CHADEMA,aliyeshindwa kutetea kiti hicho , aliyepata kura 27,332.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad