UCHAGUZI MKUU TANZANIA 2015:-Rais JK amepiga Kura Chalinze na hii ndio mipango yake akistaafu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, October 25, 2015

UCHAGUZI MKUU TANZANIA 2015:-Rais JK amepiga Kura Chalinze na hii ndio mipango yake akistaafu.

Rais waTanzania anayemaliza muda wake,Dr. Jakaya Mrisho Kikwete nae ameungana na Watanzania kuhakikisha anatimiza haki yake kama Raia wengine kwa kupiga Kura yake leo October 25,2015 katika uchaguzi mkuu wa Taifa la Tanzania, kuchagua Rais,Wabunge na Madiwani, watakao unda Serikali ya awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2X6A0562
Kuna vituo vya TV vinarusha Live matangazo ya Uchaguzi Mkuu leo, Rais Kikwete kapata nafasi ya kuongea machache baada ya kupiga Kura katika Kijiji cha Msoga, nyumbani kwao Chalinze Mkoa wa Pwani.

Nimefurahi nimepata nafasi yangu kwa kupiga Kura, naomba zoezi liwe salama… natamani Vituo vyote viwe tulivu kama hiki cha Msoga” – Rais Jakaya Kikwete.
Vipi kuhusu Ushindani wa Uchaguzi wa mwaka 2015 anavyoona? >>> “Miaka yote ushindani umekuwa mkali, nimeshiriki Uchaguzi 2005 na 2010, ulikuwa mkali tu !!“>>> Rais JK.

Mipango yake baada ya kustaafu je? >>> “Nitakuwa Rais Mstaafu, mimi ni mfugaji na ni mkulima… Baada ya hapo nitaanzisha Taasisi ya Maendeleo itakayosaidia Tanzania na Afrika na Dunia… Tarehe tano nitakuwa Rais Mstaafu.”>>> Rais Jakaya Kikwete.
2X6A0582    2X6A0578 2X6A0576

2X6A0621
Sauti ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete hii hapa mtu wangu…BOFYA HAPA KUMSIKILIZA.


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad