UCHAGUZI MKUU 2015- JIMBO LA NGARA:-Ni ushindi wa Mafuriko wa CCM kwa Bw. Alex Gashaza akishinda kwa asilimia 53. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, October 26, 2015

UCHAGUZI MKUU 2015- JIMBO LA NGARA:-Ni ushindi wa Mafuriko wa CCM kwa Bw. Alex Gashaza akishinda kwa asilimia 53.

Mgombea  ubunge wa Jimbo la Ngara Mkoani kagera  kwa tiketi ya Chama cha mapinduzi ,Bw.Alex Rafael Gashaza,akisaini karatasi ya matokeo jioni ya leo October 26,2015 katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera.

 Mgombea huyo wa Chama cha Mapinduzi, ametangazwa kushinda Ubunge wa Jimbo la Ngara, kwa kupata  kura 53,387 sawa na 53.11% dhidi ya kura halali 90,078 zilizopigwa.


Msimamizi wa Jimbo la uchaguzi la Ngara,mkoani  Kagera ,Bw.Kevin Makonda, amesema Bw.Gashaza amemshinda mpinzani wake wa karibu  Dr Bujari Peter Simon (CHADEMA/UKAWA) aliyepata kura 35,254 sawa na asilimia 39.11.

Bw.Makonda amesema wagombea wengine ni Bi. Helen Adrian Gozi (NCCR - Mageuzi), aliyepata kura 997 sawa na 1.11%  pamoja na Bw.Dotto Jasson Bahemu wa chama cha ACT Wazalendo aliyepata kura 440 sawa na 0.49%.

Amesema  Jimbo hilo la Ngara liliandikisha wapiga kura 126, 795, waliopiga kura ni 92,389 ambapo kura 2,311 ziliharibika,huku  wagombea Udiwani zilikuwa ni kata 22 , na Kata zote 21 zikienda  CCM dhidi ya  vyama vya  ACT Wazalendo na CHADEMA huku Kata ya Kasulo uchaguzi wake Ukiahirishwa kutokana na Kifo cha Mgombea wa chama cha ACT Wazalendo ,Marehemu Seif Mporogomi.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad