Mratibu
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro
Rodriguez akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu
maandalizi ya sherehe za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa pamoja na kutolea
ufafanuzi malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs) yenye lengo la kufuta
kabisa umaskini.(Picha zote ne Geofrey Adroph wa Pamoja Blog).
Naibu
Katibu Mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Balozi Hassan Simba Yahya akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) kuhusu maadhimisho ya kuundwa kwa Umoja wa Mataifa
yatakayofanyika siku ya Jumanne Tarehe 13, Oktoba 2015, katika viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja
wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez.
Baadhi
ya Maofisa wa Umoja wa Mataifa na maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa wakiendelea kufuatilia yanayojiri kwenye
mkutanoni na waandishi wa habari.
Waandishi wa habari wakifuatilia kinachoendelea mkutanoni.
Mratibu
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro
Rodriguez (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine
Mushy (kulia) wakiwa wameshikilia lengo namba 1 na 13 kati ya malengo
17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.
Mwanafunzi
wa shule ya msingi ya Agha Khan, Iman Kawambwa akiwa ameshikilia lengo
namba 4 kati ya malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.
Wafanyakazi
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa
wameshikilia lengo namba 5 na 10 kati ya malengo 17 ya Maendeleo
Endelevu ya Dunia.
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu akiwa ameshikilia lengo namba 17 kati ya malengo 17 ya Maendeleo
Endelevu ya Dunia.
Afisa
Habari wa Shirika la kazi duniani (ILO) Tanzania, Magnus Minja na
Afisa habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella
Vuzo wakiwakilisha lengo namba 1 na 8.
Baadhi ya wandishi wa habari wakiwa wameshika namba mbalimbali za malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.
Na Mwandishi wetu
Kila
Oktoba 24 ya kila mwaka, Umoja wa Mataifa huadhimisha siku ya kuundwa
kwake. Kwa mwaka huu Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania
yanayofanya kazi kama taasisi moja yameendelea kujishughulisha na kazi
mbalimbali za kijamii zenye lengo la kuadhimisha miaka 70 ya kuundwa kwa
umoja huo.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini
na Mwakilishi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez kuhusu umuhimu wa malengo
hayo amesema "Kwa hakika maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa ni
wito wa kujitazama, kuona yale tuliyofanya kwa miongo kadhaa na
kujikita kuona namna ya kuabiliana na umaskini hapa nchini Tanzania na
Duniani kwa ujumla
"Malengo
ya Maendeleo endelevu ni wito wa kuwajibika kwetu sote. Hakuna mtu
anayeweza kufanikiwa akiwa peke yake.
Inabidi tufanye kazi kwa
pamoja,wadau wote,serikali na bunge, vyama vya kiraia, madhehebu ya
kidini, wafanya biashara, wajasiliamali, na wanazuoni.Na hakika
tukishirikiana kwa nguvu pamoja na amani tunaweza kufikia malengo ya
maendeleo endelevu"
Pia
alisistiza kuwa “Malengo ya dunia yaliyojengwa katika Malengo ya
Milenia yamelenga kukabiliana na matatizo ya zamani kwa mbinu mpya.
Zimelenga
kukabiliana na tatizo la umaskini na ukosefu wa usawa katika masuala ya
uchumi. SDGs haiwezi kufanikiwa bila kuyaangalia masuala ya mabadiliko
ya tabia nchi, usawa wa jinsia, haki za biandamu na kukabiliana na mfumo
inayobagua.”
Akizungumzana
waandishi wa habari Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya amesema kuwa
nia ya serikali ni kuendelea kushirikiana na mashirika ya umoja wa
mataifa na kuwatakawatengeneze sera nzuri ambazio zitahakikisha hakuna
mtu anayeachwa nyuma katika mipango ya maendeleo ya kitaifa.
Aliendelea
kufafanua kwa kusema Tanzania inafurahishwa na ukweli unaoonekana
kwenye malengo mapya ya maendeleo endelevu kwani yamechota pia yale
malengo ya milenia ambayo yalikuwa bado hayajamaliziwa kwani katika hayo
kunaweza kuleta mabadiliko ya kuwezesha kuondokanana umaskini katika
sura zake zote ifikapo mwaka 2030.
Maadhimisho
ya Umoja wa mataifa yatafavyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini
Dar es Salaam siku ya Jumanne Oktoba 13 badala ya siku iliyozoelekaya
Oktoba 24 ili kupisha uchaguzi mkuu wa Tanzania unaofanyika Oktoba 25.
Na kauli mbiu ya maadhimisho ya Umoja wa mataifa mwaka huu ni "Umoja wa
Mataifa uliothabiti, Dunia bora".
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
No comments:
Post a Comment