Mkuu wa wilaya ya Karagwe,Mkoani Kagera,Bw. Deodatus
Kinawiro amesema kuanzia wiki ijayo Tani 40 za mahindi
zitaanza kugawiwa kwa waathirika wa maafa ya mvua zilizonyesha
Agosti 31 na Septemba 03 mwaka huu katika kata za
Kihanga,Kanoni ,Igurwa na Kidogo kwa Kata ya Bugene.
Amesema kuwa walikuwa wameomba Tani 48 za mahindi na Tani 16 za Maharage kwa wilaya ya Karagwe lakini wamebahatika kupata mahindi tani 40 ambazo zimepatikana tayari hivyo amewataka wananchi kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa.
Bw. Kinawiro ambaye sasa anakaimu wilaya ya Ngara , amesema wilaya ya Ngara nayo imepata tani 40 za Mahindi kutokana na maafa yaliyosababishwa na mvua hivyo wananchi wavute subira maana mahindi yanasafirishwa kutoka ghaLa ndogo iliyopo Shinyanga.
Pia amewashukuru wananchi ambao waliwasitiri wenzao kwa kipindi cha maafa na wengine walitoa hata misaada ya vyakula na imedhihilisha Tanzania ni nchi ya amani upendo na mshikamano.
Amesema serikali ya wilaya ya Karagwe inao mkakati wa kuwaelimisha wananchi kubadili mazoea ya kutegemea migomba kwa ajili ya kupata chakula chao kikuu ambacho ni ndizi na badala yake wabadilike waanze hata kura ugali na kulima zao mengine kama mbadala wa migomba.
No comments:
Post a Comment