KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2018:-Matokeo ya mechi ya Taifa Stars Vs Malawi Leo October 07,2015. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, October 07, 2015

KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2018:-Matokeo ya mechi ya Taifa Stars Vs Malawi Leo October 07,2015.

October 07,2015 ni siku ambayo timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ilishuka dimbani kucheza mechi ya hatua za awali za kuwania kufuzu kucheza michuano ya Kombe la Dunia 2018. Huu ulikuwa ni ufunguzi rasmi wa kuanza kwa hatua za awali za mechi hizo. Taifa Stars inayofundishwa na Charles Boniface Mkwasa ilianza kampeni yake kwa kucheza na timu ya taifa ya Malawi.
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Shomary Kapombe, Mwinyi Hajji, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Himid Mao, Thomas Ulimwengu/Ibrahim Hajib dk86, Said Ndemla, Mbwana Samatta, Mrisho Ngassa/Salum Telela dk69 na Farid Mussa/Simon Msuva dk80.
Kikosi cha Malawi; Simplex Nthala, Stanley Sanudi, Mivale Gabeya, Yamkani Fadya, Limbikani Mzava, Gerald Phiri, Chimango Kayira, Micium Mhone/Mamase Chiyasa dk46, Chawangiwa Kawanda, John Banda/Gabadinho Mhango dk58 na Robin Ngalande. 



Timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars leo October 07,2015, imeshinda ya mechi ya kwanza mwaka huu, baada ya kuilaza Malawi mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza wa mchujo kuwania kupangwa makundi ya kugombea tiketi ya Kombe la Dunia Urusi mwaka 2018.

Magoli ya Taifa Stars yalifungwa na Mbwana Samatta dakika 19 na Thomas Ulimwengu dakika ya 22 .

Kwa ushindi huo, Taifa Stars iliyocheza mechi 11 bila ya ushindi mwaka huu, nane chini ya kocha aliyeondolewa, Mholanzi, Mart Nooij, imejiweka katika nafasi nzuri ya kusonga hatua ya mwisho ya mchujo, ambako itamenyana na Algeria.  

Taifa Stars ambayo inafundishwa na mzalendo Charles Boniface Mkwasa, sasa itahitaji kwenda kulazimisha sare katika mchezo wa marudiano Jumapili mjini Blantyire,Jumapili ya October 11,2015.

Taifa Stars ambayo ilikuwa na nyota wake wote hadi wanaocheza soka la kulipwa katika nchi za Afrika Kusini na Congo, imeingia ikiwa na rekodi ya kufanya vizuri katika mechi yake ya mwisho dhidi ya Nigeria kwa kutoka bila kufungana na mabingwa hao wa zamani wa Kombe la mataifa ya Afrika.

 Taifa Stars katika Viwango vya FIFA ipo nafasi ya 136 wakati Malawi wakiwa nafasi ya 101...Picha zote kwa Hisani ya MILLARDAYO.COM

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad