Jeneza la
mwili wa Mchungaji Mtikila likishushwa viwanja vya Karimjee kwa kuagwa.
|
Rai wa
Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete akisaini katika kitabu cha
maombolezo.
|
Makamu wa
Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal akisaini kwenye kitabu cha maombolezo.
|
Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari, Maalim Seif Hamad Sharif
akisaini kitabu cha maombolezo.
|
Rais Kikwete
(katikati) akiwa kwenye msiba huo kabla ya kuuaga mwili wa Mch.Christopher
Mtikila sambamba na viongozi wengine.
|
Waombolezaji
wakihuzunika wakati wa kuuaga mwili…KWAPICHA
ZAIDI BOFYA.
RAIS wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wake, Dk.
Mohammed Gharib Bilal na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Maalim Seif Hamad wamejitokeza leo kwenye viwanja vya Karimjee jijini
Dar es Salaam kutoa heshima zao mwisho kwenye mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa
Democratic Party, Mchungaji Christopher Mtikila.
Marehemu
Mtikila alikuwa mwanasiasa mkongwe aliyefariki dunia kwa ajali ya gari Oktoba 4
mwaka huu katika Kijiji cha Msolwa, Chalinze
Mkoa wa Pwani, wakati akirejea Dar es Salaam kutokea Njombe alikokuwa
amekwenda kufanya mkutano wa kampeni.
Viongozi wa
vyama vya siasa, taasisi na mashirika mbalimbali yalipata fursa ya kutoa
shukurani zao za pekee kuzungumzia historia ya marehemu enzi za uhai wake
ambapo kila mmoja alimzungumzia
Mchungaji Mtikila alivyokuwa kiongozi shujaa, mwenye maamuzi na
kusimamia kile alichokuwa akikiamini.
Akitoa
salamu za rambirambi Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini Jaji, Francis Mutungi
amesema kuwa marehemu ameacha pengo kubwa kwa chama cha DP, kwani alikuwa
kiongozi aliyekuwa akisimamia haki na kile alichokuwa akiamini na alikuwa
hapindishwi na mtu yeyote na alikuwa ni mmoja wa wanaharakati wa haki za
binadamu.
Alisema kuwa
Mtikila alikuwa mwanaharakati asiyependa maandamano mwenye kuchukua maamuzi ya
kwenda mahakamani kwa ajili ya kupata haki anayoitaka na ndiye alikuiwa
mwanzilishi wa kudai mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.
Mwili wa
marehemu umesafilishwa kwenda Ludewa, Njombe ambapo wakazi wa mkoa huo watapata
nafasi ya kutoa heshima zao za mwisho kabla ya kuzikwa. Anatarajiwa kuzikwa
kesho.
NA DENIS
MTIMA/GP
|
No comments:
Post a Comment