Katibu
Mkuu wa Baraza la Mahedhebu kwaajili ya Amani,Mchungaji,Canon Thomas
Godda akizungumza katika kongamano la Amani lililoandaliwa na shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,Sayansi na Utamaduni
(UNESCO)kwa kushirikiana na madhehebu ya Dini na Viongozi wa Mila ili
kuhamasisha amani katika kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Na Mwandishi wetu, Simanjro
Shirika
la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia na Sayansi, Elimu na Utamaduni
(UNESCO) limekutanisha wadau mbalimbali katika kongamano la kujadili na
kuhamasisha amani katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu
unaotarajiwa kufanyika Oktoba 4,2015.
Kongamano
hilo lilifanyika katika Kituo cha Redio Orkonerei (ORS)Terrat wilaya ya
Simanjiro mkoa wa Manyara na kuwaleta pamoja viongozi wa dini,mila na
wawakili wa muungano wa Redio za Jamii nchini(Comneta)ambao kwa pamoja
walisisitiza umuhimu wa amani.
Ofisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph alisema
mchango wa unaotolewa na Redio za kijamii nchini ni mkubwa kwani
unawawezesha wananchi kuzitumia kujiletea maendeleo katika nyanja
mbalimbali ikiwemo ya kuhamasisha amani na utulivu katika kipindi hiki
na baada ya uchaguzi mkuu.
Ameongeza
kuwa Muungano wenye nguvu wa Redio za Jamii ndio ukombozi wa wananchi
kwani wanahitaji kuelimishwa maswala mbalimbali ya afya, kilimo na
programu zinazoandaliwa na serikali kwajili ya wananchi.
Mmoja
wa viongozi wa mila ,Laigwanani Lesira Samburi alisema viongozi wa mila
licha ya mchango wao kwenye jamii bado hawajashirikishwa ipasavyo
pamoja kuwa huwa hawajishughulishi na siasa moja kwa moja.
"Naomba
serikali itambue mchango wetu katika kutatua migogoro na kuhamasisha
amani kwenye jamii zetu,tunaweza kufanya mambo makubwa kama serikali
ikitushirikisha ipasavyo sio katika kipindi hiki cha uchaguzi tu bali
hata baada ya uchaguzi,"alisema Samburi
Mwenyekiti
wa Radio za Jamii kutoka UNESCO na Mhadhiri Mwandamizi wa Mawasiliano
katika Chuo Kikuu cha Hyderabad, Profesa Vinod Pavarala akizungumza
katika kongamano la amani, lililofanyika katika Kituo cha Redio ya Jamii
ya ORS (OPA)iliyopo wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara.
Pichani wanaofatilia kwa karibu ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Dini kwa
ajili ya Amani, Mchungaji Thomas Godda na Afisa Miradi wa UNESCO,
Al-Amin Yusuph.
Nae
Katibu Mtendaji wa Baraza la Dini kwaajili ya amani, Mchungaji Thomas
Godda alisema viongozi wa mila wana michango muhimu kwani wako karibu
sana na jamii inayowazunguka hivyo wakishirikiana na viongozi wa
madhehebu ya dini na asasi za kiraia kuna mambo ya msingi yatakayoipa
jamii heshima .
Alisema
Tume ya uchaguzi imewashirikisha katika hatua muhimu wadau wake
kuhakikisha kila mwananchi aliyejiandikisha anapata haki ya kupiga kura
na hakuna udanganyifu utakaotokea hivyo kuwataka wananchi washiriki kwa
amani tukio hilo muhimu katika kukuza demokrasia nchini.
Mjumbe
wa bodi ya Muungano wa Redio za Jamii nchini (COMNETA), Balozi
Christopher Liundi alisema iwapo wananchi watazitumia ipasavyo redio za
jamii zitaleta mabadiliko chanya.
Mjumbe
wa Bodi ya Muungano wa Redio za Jamii nchini (COMNETA), Balozi
Christopher Liundi akichangia mada ya umuhimu wa matumizi ya Redio za
Jamii.
Kiongozi
wa Mila ya jamii ya wafugaji katika Kijiji cha Terrat wilaya Simanjiro
mkoa wa Manyara, Lesira Samburi akizungumza kwenye kongamano la
kuhamasisha amani kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini wa Redio ya Jamii 94.9 Mkoani,Pemba,Hamdu Hasan
Bakari (kushoto)akiteta jambo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Dini kwa
ajili ya Amani, Mchungaji Thomas Godda.
Meneja
wa Orkonerei Radio Service Simanjiro Manyara (ORS FM), Bw. Baraka Ole
Maika akivishwa Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika
la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin
Yusuph mavazi ya jamii ya wafugaji wa kimaasai ikiwa ni ishara ya
kumpongeza na kumuaga baada kuhamishwa kikazi nchini India, kushoto ni
Mwenyekiti wa Muungano wa Redio za Jamii nchini (COMNETA), Joseph
Sekiku.
Ofisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph (kulia)
akifurahia zawadi ya mavazi na Rungu la jamii ya wafugaji wa kimaasai na
kusimikwa rasmi kuwa 'Laigwanan' kwa kutambua mchango wake katika
kuendeleza jamii hiyo kupitia Redio za jamii nchini, Al Amin amepewa
uhamisho kwenda India, kushoto ni Kiongozi wa Mila, Laigwanan Lesira
Samburi na Mwenyekiti wa Muungano wa Redio za Jamii (COMNETA) Sekiku
Joseph.
Viongozi wa Mila wakionesha ujumbe wa kuhamasisha amani.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Dini kwaajili ya Amani, Mchungaji Thomas Godda
(kushoto) akiteta jambo na maafisa wa UNESCO, Nancy Kaizirege na Al
-Amin Yusuph.
Ujumbe
wa Muungano wa Redio za Jamii,Wazee wa Mila na Viongozi wa dini
wakiwasili kwenye kiwanda cha kuzalisha nishati kwa njia ya Mibono
katika Kijiji cha Terrat ambacho kimekua msaada kwa wananchi wengi.
Mkurugenzi
wa Kituo cha Redio ya Jamii ya ORS (OPA)iliyopo wilaya ya Simanjiro
mkoa wa Manyara,Martin Kariongi (kushoto) akizungumza na ujumbe
ulioshiriki kongamano la amani lililoandaliwa na Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshighulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
waliotembelea mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia teknolojia ya Mafuta
ya Mibono.
No comments:
Post a Comment