Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa
Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akifungua warsha ya vijana na
ajira iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti ya Maendeleo ya
Kimataifa kutoka Canada (IDRC). Kushoto ni Meneja Ajira za Kifundi kwa vijana
na Mratibu Kazi wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) Dk. Annmarie Kiaga na
kulia ni Kiongozi Mpango wa Ukuaji na Ajira wa Taasisi wa Mpango wa Shirika la
Utafiti ya Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) Dk. Arjan de Haan.
Naye Mungu akatabsamu akamwambia, Joseph, si
ununue tiketi basi?
Dk Kiaga alisema kwa kuzingatia hadithi yake
kila mmoja anatakiwa kufanya kitu na Joseph alisahau kwamba huwezi kushinda
bahati nasibu bila kununua tiketi.
“Kumbuka haitoshi kuwa na elimu na ujuzi kama
hutaweza kuweka elimu hiyo au ujuzi ulionao katika vitendo” alisema na kuongeza
kuwa Joseph alikuwa anajua anahaitaji fedha ya kianzio lakini hakuchukua hatua
ya kupata hela hiyo.
Alisema pamoja na ukweli kuwa asilimia 40 ya
watu wasio na ajira duniani ni vijana, kwa maana ya kwamba kuna vijana
wapatao milioni 75 duniani kote wanatafuta ajira huku vijana wa kike wakiwa na
changamoto kubwa zaidi, ipo shida kubwa ya vijana kukata tamaa.
Aidha alisema kwamba hali ya kukata tamaa
imewapeleka vijana kuongezeka katika soko la vijana wanaopata kazi zisizo na
staha.
Alisema pamoja na sera zilizopo vijana
wanatakiwa kuwa na shauku na kazi na pia kujitambua.
“Vijana wa siku hizi hawana mitazamo sahihi
kuhusu ajira. Kwamba vijana hawana shauku na kazi na wana mitazamo hasi (ili
mradi kazi..mkono uende kinywani?) . Matokeo yake ni kwamba vijana hawatumii
ubunifu wowote katika kuboresha uwezekano wao wa kupata kazi zenye staha”
alisema.
Amesema mtaji unahitaji kujiboreshea seti ya
ujuzi katika kutafuta kazi ikiwa ni pamoja na uwezo, uzoefu na elimu.
|
Meneja Ajira za Kifundi kwa vijana na Mratibu
Kazi wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) Dk. Annmarie Kiaga akizungumza
kwenye warsha ya vijana na ajira iliyofadhiliwa na Mpango wa
Shirika la Utafiti ya Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) na kuratibiwa
na ESRF.
Alisisitiza kuwa vijana waliowengi
hawajitambui na kujiuliza ‘mimi ni nani’ au hawana malengo binafsi na matarajio
mimi nataka kuwa nani na kusema bila kuyafanyia kazi mambo hayo mawili ya
shauku ya kazi na kujitambua hakutakuwepo na mabadiliko.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida, akifungua warsha hiyo
alisema pamoja na taifa kuwa mstari wa mbele kushughulikia ajira kwa vijana kwa
kutunga sera zilizolenga kukidhi haja ya ajira,ikiwemo Sera ya Taifa ya
Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007, Sera ya Taifa ya Ajira ya mwaka 2008 na na
mpango wa utekelezaji wa sera ya taifa ya ajira kwa vijana iliyo chini ya
mtandao wa ajira unaofadhiliwa na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa,
changamoto bado zipo.
Aliwataka washiriki wa warsha hiyo wakiwemo
vijana waliofanikiwa kueleza siri za fursa na kujiajiri ili kutoa mwanga kwa
wenzao.
Pamoja na warsha hiyo kutoa nafasi kwa
vijana kujadili namna ya kutambua na kutumia fursa za kuichumi zilizopo nchini,
kutoa ujuzi kwa vijana wa namna ya kuingia katika soko la ajira ikiwa ni
pamoja na kujiajiri, kukuza ujasiriamali na kuendeleza biashara, Dk Kida aliwasihi
vijana kujitafutia riziki yake na kushiriki ipasavyo katika shughuli za
kiuchumi na maendeleo.
Aliwataka kujijengea uwezo wa kufanyakazi
pamoja na kubaini na kuzitumia fursa za kiuchumi na kibiashara zilizopo nchini.
Warsha hiyo iliyofadhiliwa na Mpango wa
Shirika la Utafiti ya Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) ilikutanisha
vijana kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania na kuwezeshwa kwa sehemu kubwa
na Taasisi ya tamasha ambapo Mkurugenzi wake Mtendaji Richard Mabala alikuwa
Mchokozaji mkuu.
Akiwasilisha salamu kutoka IDRC, kiongozi
Mpango wa ukuaji na ajira wa taasisi hiyo. Dk Arjan de Haan alisema kwamba
taasisi hiyo ya serikali ya Canada imekuwa ikitoa ushirikiano katika tafiti
zilizolenga kuangalia utatuaji wa tatizo la ajira kwa namna inavyofaa.
|
Mtafiti Mwandamizi ESRF, Dk. Georgina Ole
Saibul akiwasilisha mada katika semina ya vijana na ajira.
Alisema kwamba kwa kawaida taasisi yake
husaidia pale inapoona utafutaji wa mbinu za kutatua tatizo unashirikisha na
wahusika ili kupata suluhu endelevu ya tatizo husika.
Alisema ameridhishwa na kuona kwamba warsha
hiyo imezingatia kanuni za IDRC za kutaka kutatua tatizo la ajira kwa
kushirikisha vijana wenyewe, kuangalia na kushauri namna bora ya kukabili
tatizo la ajira ambao kwa sasa ni changamoto kubwa duniani.
Alisema kwamba ipo haja ya kubadili baadhi ya
sera kulingana na mahitaji ya sasa ili kuwezesha vijana wengi zaidi kuingia
katika soko la ajira.
Wakati wa utambulisho na kuelezea kero zao
katika ajira wengi wa vijana waligusia kuwapo kwa sera ambazo si rafiki
zinazotengeneza urasimu mkubwa katika kusaidiwa.
Ingawa wengi walisema fursa zipo,
walizungumzia kutopata ushirikiano kutoka kwa wazazi , viongozi na taasisi
mbalimbali zinazodai kupambana na ukosefu wa ajira kwa vijana.
Aidha vijana wengine walisema kwamba ni kweli
kuna mtazamo hasi kwa vijana hasa kukata tamaa na pia kutaka maendeleo ya kasi
huku wakikosa ubunifu.
Joachim Fanuel kutoka singida Youth
Entrepreneurs and Consultants Cooperative Society (SYECLOS) alisema kwamba
ingawa wao wanaendesha miradi ya kuku wa kienyeji na asali kama fursa zilizopo
wanakabiliwa na tatizo la kukata tamaa kutokana na kuona kwamba inachukua muda
mrefu kupata vitu wanavyotaka.
Aidha alisema kwamba wamekuwa hawasikilizwi
na serikali na taasisi mbalimbali kwa kuwa hawana mali za kuwakilisha kama
dhamana katika mambo mbalimbali.
|
Johari A. Sadik kutoka kampuni inayotengeneza
nguo za kitamaduni Binti Africa, akitoa ushuhuda kwamba vijana
wanaweza kama watajitambua katika warsha ya siku mbili vijana na ajira inayofanyika
hoteli ya DoubleTree by Hilton.
Kijana Musa Mohammed kutoka Zanzibar
alisema kwamba japo wana fursa za usindikaji wa vyakula, mizizi na matunda
wamekuwa na tatizo la ujuzi katika uchakataji, sera duni zisizojibu mahitaji
yao na kuwalinda katika soko.
Binti mmoja kutoka Binti Africa Kampuni
inayotengeneza nguo za kitamaduni alisema kwamba kuna shida ya kukata tamaa
miongoni mwa vijana lakini pia hawajali kutafuta taarifa wanazohitaji
wakisubiri kutafuniwa.
Vijana wengine walizungumzia ugumu wa mitaji,
ukosefu wa taaluma na mfumo wa elimu kwuatengeneza kupata ajira katika serikali
na taasisi zake.
Mshiriki Leticia Mango kutoka Kigoma
alisema kwamba ipo shida ya vijana wenye vipaji ambao hawana elimu vijijini
kudharaulika na kutothaminiwa kwa kile kinachoonekana sio wasomi.
Alisema vijana wasomi wakiunganika na wenye
vipaji wanaweza kuwa mbali zaidi na kusisitiza ipo haja vijana kuwa pamoja kwa
maendeleo yao.
|
Joachim
Fanuel kutoka Singida Youth Entrepreneurs and Consultants Cooperative Society
(SYECCOS) akionesha chupa ya asali kutoka kwa mradi wa kikundi cha vijana ambao
waliamua kujiajiri katika warsha ya vijana na ajira.
|
Joachim
Fanuel kutoka Singida Youth Entrepreneurs and Consultants Cooperative Society
(SYECCOS) akizungumza na washiriki wa
warsha ya vijana na ajira.
|
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida
(kushoto) akiwa na Kiongozi Mpango wa Ukuaji na Ajira wa Taasisi wa Mpango wa
Shirika la Utafiti ya Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC), Dk. Arjan de
Haan wakiwa katika warsha ya vijana na ajira.
|
Vijana wakishiriki kazi za vikundi kwenye warsha hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida
akiwa katika picha ya pamoja na vijana walioshiriki warsha ya vijana na
ajira hoteli ya Double Tree by Hilton
jijini Dar.
|
No comments:
Post a Comment