|
Kwa mujibu wa waziri huyo..‘Mtakumbuka kwamba mwezi mmoja hivi uliopita nilikutana nanyi
kuwapa taarifa juu ya maendeleo ya mradi wa bomba la gesi na mitambo ya
kuzalisha umeme kwa gesi pamoja na majaribio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea
katika mifumo hiyo‘ – George Simbachawene |
|
‘Mtakumbuka kwamba mwaka 2012 serikali ilianza mchakato wa
kutekeleza mradi mkubwa wa bomba la gesi ambalo kukamilika kwake kungesaidia
sana kuondoa matatizo ya umeme nchini.Kazi hiyo ilijumuisha ujenzi wa mtambo wa
kuchakata gesi wa madimba (Madimba Processing Plant), mtambo wa kuchakata Gesi
wa Songosongo (SongoSongo Processing Plant) na Bomba kubwa la kusafirisha gesi kutoka
Mtwara na kuja Dar es Salaam‘ – George
Simbachawene
|
‘Hata hivyo mitambo iliyoanza kuzalisha umeme ni ya Megawati 90
tu kwa sasa. Tunaendelea kufuatilia ufanisi wa bomba na hasa msukumo wa gesi
pamoja na vigezo vingine vya kitaalamu kabla hatujawasha mitambo mingine.Hii ni
kwasababu mfumo wote wa bomba ni mpya na tunapoigiza mitambo hii inabidi
tuiingize kwa uangalifu kuepusha madhara katika mfumo wa bomba’ – George Simbachawene
|
‘Sambamba na hilo,, kila mtambo una kiwango chake cha msukumo
wa Gesi kinachoruhusu mtambo husika kuwaka, hivyo kwa kadri viwango vya msukumo
wa Gesi katika Bomba vinavyozidi kuimarika ndivyo uzalishaji wa umeme
utakavyoendelea kuongezeka.Hii ina maana kwamba upungufu wa umeme uliokuwepo
utaendelea kupungua hatua kwa hatua kulingana na mitambo hii inavyoendelea
kuwashwa na kuzalisha umeme’ – George Simbachawene
|
Msafara wa
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene...Picha zote Na:-MILLARDAYO
|
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630. |
No comments:
Post a Comment