Hii
ilitengenezwa Ufaransa. Ni ndogo sana, inaweza kuruka kwa saa mbili tu katika
nusu kipenyo cha kilometa 15 kutoka ilipo mitambo.
DT-26
ilijaribiwa Selous
|
Imetengenezwa
Ufaransa na kampuni ya Delair Tech. Hii ni kubwa kidogo, ina uwezo mkubwa na
inatumia viwango vya satelaiti za kijeshi vya mawasiliano kutumana
kupokeataarifa pamoja na namna ya kuongozwa kwake.
Superbat DA
50 – Imejaribiwa Mkomazi
|
“Sasa hapa
unaweza kuona kama kuna wavamizi (majangili) na inakuwa rahisi kuwasiliana na
askari wa wanyama pori na kwenda kwenye eneo husika kuwakamata,” anasema Jones.
Hata
ilipotua, ilikuja kama ndege za kawaida zinavyokuja, tofauti yake tu yenyewe
haina magurudumu. Naam, unaweza kuwa ufumbuzi mwingine wa kupambana na ujangili
nchini, tatizo ambalo haliko Tanzania tu, bali katika nchi nyingi barani
Afrika.
Taasisi
mbalimbali za ndani na nje zikiwemo serikali za mataifa makubwa zimekuwa
zikijitahidi kusaidia mapambano hayo kama alivyofanya Rais Barack Obama wa Marekani
alipoahidi kutoa Dola milioni 10 (sawa za Shs. 20 bilioni) ili kuimarisha
mapambano hayo nchini.
Takwimu
zinaonyesha kuwa Bara la Afrika mwaka 1930 lilikuwa na tembo 50 milioni na
kwamba hadi kufikia mwaka 2013 tembo waliobakia katika bara zima ni 500,000.
Aidha,
takwimu hizo zinaonyesha kwamba katika miaka ya 1960 Tanzania kulikuwa na tembo
kati ya 250,000 hadi 300,000 na kwamba wanyama hao walipungua hadi kufikia
130,000 mwaka 2002 na idadi ya tembo hapa nchini imeendelea kupungua kwa kasi
ambapo hivi sasa takwimu zinaonyesha kuwa inakadiriwa kuna tembo wasiozidi
55,000.
Kwa mujibu
wa takwimu zilizopo, wastani wa tembo 30 huuawa kijangili kila siku ikiwa ni
sawa na tembo 850 kwa mwezina zaidi ya tembo 10,000 wanauawa kila mwaka,hali
ambayo inatishia uwepo wa wanyama hao wakubwa zaidi duniani kwa sasa.
Kwenye
Hifadhi ya Tarangire, jumla ya tembo 104 waliouawa katika kipindi cha miaka
mitatu tu kutoka mwaka 2007 hadi 2009 na katika Hifadhi ya Serengeti idadi ya
tembo imepongua kutoka 2,500 mwaka 1985 hadi kufikia 500 mwaka 2012 huku nyati
wakipungua kutoka 70,000 hadi 40,000 ujangili huo ukiua faru wengi kutoka 1,000
waliokuwepo mwaka 1985 hadi 20 tu.ZAIDI BOFYA HAPA KUSOMA NA KUTAZAMA PICHA PIA.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo
na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia
tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment