UCHAGUZI MKUU 2015 TANZANIA:-Tume yaamua rufaa za Wagombea. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, September 10, 2015

UCHAGUZI MKUU 2015 TANZANIA:-Tume yaamua rufaa za Wagombea.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesikiliza na kuamua rufaa rufaa 6 za wabunge kati ya rufaa 13 zilizokuwa hazijafanyiwa maamuzi kutokana na vielelezo vyake kutokamilika. Kati ya rufaa hizo, Tume imezikataa sababu za rufaa zote na kukubaliana na uamuzi wa Wasimamizi wa Uchaguzi. Hii ina maana kuwa maamuzi yaliyofikiwa na Wasimamizi wa Uchaguzi wa Majimbo husika ndio utakaofuatwa. (Jedwali 1).

 Aidha, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesikiliza rufaa za Madiwani 70 kati ya rufaa 118 zilizokuwa hazijafanyiwa maamuzi kutokana na vielelezo vyake kutokamilika. Kati ya rufaa 70 zilizoamuliwa jumla ya rufaa 14 zimekubaliwa na Tume na wagombea
waliokuwa wameenguliwa wamerudishwa kugombea. 

Hii ina maana kuwa Tume imetengua uamuzi wa Wasimamizi wa Uchaguzi na kuwarejesha wagombea katika kinyang’anyiro cha Udiwani katika Kata zao. Kwa rufaa 58 Tume imekataa sababu zilizotolewa na kukubali uamuzi wa Wasimamizi wa Uchaguzi. Hii ina maana kuwa wagombea watafuata maamuzi yaliyofikiwa na Wasimamizi wa Majimbo na Kata husika. (Jedwali 2)





Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad