TASWIRA PICHA:-Ajali ya moto yatokea katika ndege ya British Airways . - Mwana Wa Makonda
cV7ufzj

Muhtasari

X-BET

MAIN-

Post Top Ad

cV7ufzj

Thursday, September 10, 2015

demo-image

TASWIRA PICHA:-Ajali ya moto yatokea katika ndege ya British Airways .

.com/simgad/
ndege-2
Maafisa wa zima moto wakikizima moto katika ndege ya British Airways, Septemba 8, 2015 katika uwanja wa ndege wa McCarran katika mji wa Las Vegas...AFP/AFP.

ndege-5
Ndege ya shirika la British Airways imewaka moto wakati ilikua ikijianda kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Las Vegas, nchini Marekani, Jumanne wiki hii. Watu 172 waliokua katika ndege hiyo wameokolewa kwa dharura, ikiwa ni pamoja na watu saba ambao wamepata majeraha madogo.

Abiria 159 na wafanyakazi 13 wa ndege hiyo, ikiwa ni pamoja na marubani watatu pamoja na wafanyakazi wengine kumi, kwa mujibu wa shirika la British Airways ndio waliokua katika ndege hiyo.

Kwa mujibu wa akaunti ya Twitter ya mamlaka ya uwanja wa ndege wa McCarran, watu saba miongoni mwa watu waliokua katika ndege hiyo wamepata majeraha madogo.
ndege-1
Kwa mujibu wa mamlaka ya safari za ndege (FAA), tukio hilo limetokea wakati " injini ya kuhoto ya Boeing 777-200 ya British Airways iliwaka moto wakati wa ikijiandaa kuruka ", kwenda kwenye uwanja wa ndegea wa Gatwick, mjini London, nchini Uingereza.

Source:-rfi.


ndege-3

ndege-4
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *