FURSA ZA UWEKEZAJI:-Dkt. Bilal alifungua Kongamano la kuwekeza katika mikoa ya ukanda wa Ziwa Tanganyika Mjini Kigoma. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, September 10, 2015

FURSA ZA UWEKEZAJI:-Dkt. Bilal alifungua Kongamano la kuwekeza katika mikoa ya ukanda wa Ziwa Tanganyika Mjini Kigoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Uwekezaji wa Ziwa Tanganyika, lililofanyika Jana September 9, 2015 kwenye Hoteli ya Tanganyika Mjini Kigoma… Picha zote na OMR.

Makamu wa Rais Dr Mohamed Gharib Bilal , akizungumza kwenye Ufunguzi wa Kongamano hilo la Uwekezaji katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika,amebainisha kuwa kukosekana kwa Miundombinu bora ya Barabara, Reli, Maji na Anga imeathiri kwa kiasi kikubwa Maendeleo ya Ukanda wa Ziwa Tanganyika.

Amesema kukosekana kwa miundombinu imara katika ukanda huo unaojumuisha Mikoa ya Kigoma, Rukwa na Katavi kumeathiri Maendeleo na kwamba kwa sasa Serikali ya Tanzania imewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye miundombinu hiyo ili kuinua uchumi wa wakazi wa Mikoa hiyo.

Dr Bilali amewataka wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika mikoa ya ukanda wa Ziwa Tanganyika kwa kuwa kwa sasa Serikali imeweka Mkazo katika uboreshaji wa Miundombinu ili kuufungua ukanda huo.
07
Waziri wa Nchi- Uwekezaji na Uwezeshaji, Eng. Christopher Chiza, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Makamu wa Rais Dkt. Bilal ili kufungua Kongamano hilo...Picha zote na OMR
06
Mwakilishi wa Umoja wa wafanyabishara wa Burundi, akizungumza.
04
05
Sehemu ya washiriki wa Kongamano hilo wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, alipokuwa akihutubia kwenye ufunguzi wa Kongamano hilo.
02
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja ya jiwe lenye Madini huku akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Aifola Investiment Co. Ltd, Zubery Mabie, kuhusu upatikanaji wa madini na utengenezaji wa Unga wa ‘Lime Powder’, wakati Makamu alipokuwa akitembelea Mabanda ya maonesho kwenye ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji wa Ziwa Tanganyika, lililofanyika September 9, 2015, kwenye Hoteli ya Tanganyika Mjini Kigoma.
03
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wauza Samaki wa Mapambo, Nunu Mrisho, kuhusu upatikanaji wa Samaki hao na soko lake , wakati Makamu alipokuwa akitembelea Mabanda ya maonesho kwenye ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji wa Ziwa Tanganyika, lililofanyika September 9, 2015, kwenye Hoteli ya Tanganyika Mjini Kigoma.
08
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na Balozi waliohudhuria Kongamano hilo baada ya ufunguzi, uliofanyika September 9, 2015.
09
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Kigoma waliohudhuria Kongamano hilo baada ya ufunguzi, uliofanyika September 9, 2015.
010
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo waliohudhuria Kongamano hilo baada ya ufunguzi, uliofanyika  September 9, 2015.
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad