Byesige
Josephat (anayemimina mafuta) na Hezron Mtangirwa(kushoto), wakimbizi kutoka
Burundi waliohifadhiwa katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu wakipima mafuta
ili waweze kuyagawa kwa wakimbizi wenzao jana ,baada ya kugawiwa mafuta na
Shirika la Umoja wa Mataifa, linaloshughulikia chakula (WFP), ambalo lina kituo
chake katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Idadi ya
waomba hifadhi kutoka nchini Burundi katika kambi ya wakimbizi ya nyarugusu
wilayani Kasulu mkoani Kigoma imeendelea kuongezeka ambapo sasa imefikia watu
elfu 91 na 661.
Akiongea na Radio
Kwizera, mkuu wa makazi Kambini Nyarugusu, Bw Sospeter Boyo amesema kuwa idadi
ya waomba hifadhi hao inazidi kuongezeka kila siku,ambapo mpaka sasa wananaendelea kupokea waomba
hifadhi na kuwa kasi ya kuingia kwa saa ni ndogo ukulinganisha na mwezi wa sita
na wa saba, ambapo kwa sasa wanapokea waomba hifadhi chini ya 100.
Aidha Bw
Boyo amesema kuwa kwa mujibu wa waomba hifadhi hao wanakimbia nchini mwao
kutokana na mauaji ya chinichini yanayo endelea nchini mwao licha ya uchaguzi
mkuu kumalizika nchini Burundi.
|
Kinamama
wakimbizi toka Burundi wakipata mgao wao wa unga unaotolewa kwa wakimbizi
wanaohifadhiwa katika Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu
mkoani Kigoma. Serikali kwa kushirikiana
na Mashirika ya Kimataifa imeendelea kuhakikisha kuwa wakimbizi hawa toka
Burundi wanapata chakula cha kutosha kwa ajili ya mahitaji yao.
|
Mkimbizi
Irene Ntibelenda (katikati) akiwa pamoja na ndugu yake Sengiyu Mvajeme (kulia)
baada ya kupokea mgao wa chakula unaotolewa na
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia chakula (WFP), lililo na Kituo chake katika kambi ya Nyarugusu
iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma. Kushoto ni mtoto wake aitwaye
Nsengiyumva Idiphonce.
|
Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Josef Ntukugurya akifunga shehena ya unga wa mahindi jana, muda mfupi baada ya kupokea unga huo kutoka kwa Shirika la Umoja wa Mataifa, linashughulikia chakula (WFP), lililoweka kituo chake katika kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, mkoani Kigoma . |
Sehemu ya
shehena ya chakula ukiwepo unga wa mahindi na mafuta ya kupikia ikiwa katika
ghala la kuhifadhia chakula lililopo katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu
iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Chakula hiki hutolewa na Jumuiya ya Kimataifa kama kupitia Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia chakula (WFP) ili kusaidia wakimbizi
wanaohifadhiwa hapa nchini.
(PICHA NA
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI – WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI).
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo
na Nyingine kwa kujiunga na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER , INSTAGRAM , Pia
tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
|
No comments:
Post a Comment