Mkurugenzi
wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi
wa habari leo Jijini Dar es Salaam
Kuhusu Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Agosti, 2015 ambao umebaki kuwa
asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwezi Julai mwaka huu. Kushoto kwake ni Meneja wa
Idara ya Takwimu za Ajira na Bei Bi. Ruth Minja.
Na Veronica
Kazimoto
Mfumuko wa
Bei wa Taifa kwa mwezi Agosti, 2015 umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa
mwezi Julai mwaka huu.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na
Takwimu za Jamii Ephraim Kwesigabo amesema kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na
huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2015 imekuwa sawa na kasi iliyokuwepo
kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2015.
“Tunaposema
kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma ya mwezi Agosti, 2015 imekuwa sawa
na kasi ya mwezi Julai, 2015 haimanishi kuwa bidhaa hazijapanda wala kushuka
isipokuwa baadhi ya bidhaa zimepanda bei na nyingine kushuka ila kasi yake ya
upandaji bei ndio imekuwa sawa na ile ya mwezi Julai, 2015,” amesema Kwesigabo.
Kwesigabo
amefafanua kuwa kutokana na hali hiyo, Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi
kufikia 158.81 kwa mwezi Agosti, 2015 kutoka 149.31 mwezi Agosti, 2014.
Kuongezeka
kwa fahirisi za bei kumechangiwa hasa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa
zisizo za vyakula.
“Baadhi ya
bei za bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja
na gesi kwa asilimia 2.0, mafuta ya taa kwa asilimia 2.3, mazulia kwa asilimia
1.4, dizeli kwa asilimia 3.8 na petroli kwa asilimia 8.3,” amesema Kwesigabo.
Kwa upande
wa uwezo wa Shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia
Shilingi 62 na senti 97 mwezi Agosti, 2015 kutoka mwezi Septemba, 2010
ikilinganishwa na Shilingi 62 na senti 98 ilivyokuwa mwezi Julai, 2015.
Aidha,
Mfumuko wa Bei nchini una mwelekeo unaokaribiana na baadhi ya nchi nyingine za
Afrika Mashariki.
Akitolea
mfano wa nchi za Kenya na Uganda, Mkurugenzi Kwesigabo amesema Mfumuko wa Bei wa mwezi Agosti, 2015 nchini
Kenya umefikia asilimia 5.84 kutoka asilimia 6.62 mwezi Julai, 2015 na Uganda
umefikia asilimia 4.80 kutoka asilimia 5.4 mwezi Julai, 2015.
|
Wednesday, September 09, 2015

Home
HABARI
TAKWIMU ZETU:-Mfumuko wa bei wabaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwezi Julai, 2015.
TAKWIMU ZETU:-Mfumuko wa bei wabaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwezi Julai, 2015.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment