![]() |
Tukio hilo limetokea leo September
10,2015,asubuhi baada ya kichwa cha treni hiyo kutoka kwenye njia ya reli na
mabehewa ya treni kuanza kukanyaga mataluma na kusababisha adha kwa abiria hao.
Mkuu wa kituo cha reli
(Station Master) Shinyanga,Bw. Baruani Issa amesema katika treni hiyo kulikuwa
na abiria 159 na kwamba ajali hiyo imetokea kutokana na miundo mbinu ya reli
kuwa chakavu.
Station Master huyo amesema
utaratibu uliofanywa na Shirika hilo ni kufanya utaratibu wa kuwarudishia nauli
abiria hao ili wapande mabasi na kuendelea na safari zao ili kupunguza usumbufu
wakati utaratibu wa matengenezo unafanyika ili treni iendelee na safari zake
kama kawaida.
Wakizungumza na Waandishi wa Habari,Baadhi ya abiria waliokuwa wanasafiri na treni hiyo mbali na kumshukuru mwenyezi
mungu kwa kuwanusuru na ajali hiyo wameiomba serikali kuboresha miundo mbinu ya
reli kwani asilimia kubwa ya Watanzania wanategemea usafiri huo wenye gharama
nafuu.
|
![]() |
No comments:
Post a Comment